Dira |
---|
Maswali kadirifu |
- Dira ni chombo mfano wa saa.
- Dira ni chombo cha kuwaelekeza wasafiri katika pande za Dunia.
- Huwa na mshale uzungukao wenyewe.
- Hutumiwa kuonyeshea mwelekeo na hata majira.
- Dira huwa na pande nne kuu.
- Nazo ni kaskazini, mashariki, kusini na magharibi.
- Mbali na pande hizi nne, kunazo pande nyingine.
- Tazama dira ifuatayo, pande a - h hutamkwa vifuatavyo;
1) Kaskazini
2) Kaskazini kaskazini mashariki
3) Kaskazini mashariki
4) Mashariki kaskizini mashariki
5) Mashariki
6) Mashariki kusini mashariki
7) Kusini mashariki
8) Kusini kusini mashariki
9) Kusini
10) Kusini kusini magharibi
11) Kusini magharibi
12) Magharibi kusini magharibi
13) Magharibi
14) Magharibi kaskazini magharibi
15) Kaskazini magharibi
16) Kaskazini kaskazini magharibi
Ili kukumbuka kwa urahisi dhania kuwa unasema,
“Kaskazini ya kaskazini mashariki kaskazini ya kaskazini mashariki n.k”