Nyakati

- Wakati ni kipindi fulani cha muda. 

- Kwa kawaida kuna wakati wa mchana na wakati wa usiku. Mchana huanzia jua linapochomoza hadi linapozama. Mchana huupisha usiku.

- Kipindi cha usiku huendelea hadi jua linapochomoza. 

- Katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, kipindi cha mchana huchukua saa kumi na mbili sawa na kile cha usiku. Kwa jumla mchana na usiku huwa na saa ishirini na nne.

- Kipindi hiki cha saa ishirini na nne (siku moja) kinaweza kugawika katika sehemu mbalimbali kama ifuatavyo:

  • Alfajiri mbichi – mwendo kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi.
  • Mapambazuko, macheo, mawio - asubuhi jua linapochomoza; mwendo wa saa thenashara/kumi na mbili asubuhi.
  • Mafungulia ng’ombe – asubuhi mwendo wa saa mbili hadi saa tatu.
  • Adhuhuri – mchana kuanzia saa sita hadi saa tisa.
  • Jua la mtikati – saa sita mchana
  • Jua la utosini –
  • Alasiri – kati ya saa tisa mchana hadi magharibi.
  • Magharibi – wakati jua linapokuchwa/linapotua/linapozama.

  • Machweo/machwa – wakati jua linapozama.
  • Mafungianyama – jioni wakati wanyama wanaporejeshwa kutoka malishoni au machungani.
  • Wakati wa jua kuaga miti – mwendo wa jua kuzama.
  • Jioni – mwendo wa kuanzia alasiri hadi magharibi.
  • Usiku mchanga – kuanzia saa moja hadi saa tano usiku.
  • Usiku wa manane – saa saba hadi saa tisa usiku.
  • Jogoo la kwanza – mwendo wa saa tisa asubuhi.
  • Majogoo – mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.

Siku Jumla ya siku saba huwa ni wiki au juma moja.

Siku za wiki ni:

  1. Jumamosi (Sabato),
  2. Jumapili (Dominika),
  3. Jumatatu,
  4. Jumanne,
  5. Jumatano,
  6. Alhamisi,
  7. Ijumaa.

 

Mpangilio wa siku:

- Majuma manne ni sawa na mwezi mmoja. Miezi kumi na miwili ni sawa na mwaka mmoja.

- Miezi ya mwaka ni: Januari , Februari, Machi, Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba, Oktoba, Novemba, Disemba.

- Miaka kumi ni sawa na mwongo.

- Kipindi cha miaka mia moja ni sawa na karne.

- Kipindi cha miaka elfu moja huitwa kikwi au milenia.