Majira
- Majira ni kipindi kirefu kiasi cha wakati.
- Aghalabu kipindi hiki huwa na hali fulani ya hewa.
- Masika/kifuku: Majira ya mvua tele ya mfululizo.
- Kiangazi/ukame: Majira ya jua kali.
- Vuli/mchoo: Majira ya mvua ndogondogo ambazo hupatikana wakati wa pepo za kaskazi.
- Kipupwe: majira ya baridi.
- Matlai: msimu wa pepo zinazovuma kutoka mashariki.