Vitawe |
---|
Maswali kadirifu |
- Maneno yenye maana zaidi ya moja huitwa vitawe.
1. Kuwa mahali kwa muda fulani.
Mfano katika sentensi: Mama Njenga amekaa sana gulioni.
2. Kipande cheusi cha kuni kilichochomwa na kuzimwa kabla ya kuwa majivu. Hutumika kupikia kwa jiko.
Ngeli: LI - YA
Kwa wingi: Makaa
Mfano katika sentensi: Makaa yamewaka yakaisha jikoni.
3. Mnyama mdogo wa majini mwenye miguu sita au zaida, na gamba mwilini.
Mfano katika sentensi: Kakangu ametengeneza mchuzi rojorojo wa kaa.
4. Weka makalio juu ya kitu, kama vile kiti.
Mfano katika sentensi: Mtoto ameamka na kuketi kitandani.
5. Kuwa na maskani mahali.
Mfano katika sentensi: Mimi na familia yangu tunakaa Nyahururu.
1. Tamko la heshima la kumwita mtoto msichana.
2. Aina ya andazi.
1. Sehemu ya mwili.
2. Kuku wa kike aliyekomaa.
3. Familia.
1. Mnyama wa kufugwa.
2. Kifaa cha kukunia nazi.
1. Ndege mla mzoga.
2. Ukosi wa blausi au shati.
3. Aina ya vazi.
1. Pombe.
2. Ndovu.
1. Eneo la utawala/lokesheni.
2. Kutenganisha kitu kwa chombo k.v. kisu.
3. Kifaa cha kuchotea maji mtungini.
1. Kupitisha chakula kooni hadi tumboni.
2. Kifaa cha kuandalia mlo.
1. Chombo cha kutilia vinywaji k.v. maji.
2. Kuruka.
1. Mnyama jamii ya nyani.
2. Nyama iliyosagwa.
1. Kiunganishi.
2. Umbo.
1. Kuku mdogo wa kike.
2. Kidogo k.v. dawa.
3. Nyumba fupi ya udongo isiyo na paa ila dari lililotengenezwa kwa udongo.
1. Leso.
2. Teremka.
1. Kibanda cha turubali/ chandaru.
2. Tokwa na pumzi kwa nguvu.
1. Mamaye wazazi wangu.
2. Aina ya mboga.
1. Kijiji/kaya.
2. Kiti cha pili cha baiskeli cha kubebea mtu wa pili au kubebea mizigo.
3. Sehemu ya juu ya gari ya kubebea mizigo.
1. Mabaki ya jengo lililobomoka.
2. Mchezo wa magongo.
1. Mfuko wa kuwekea kisu au upanga.
2. Neno la kuonyesha mshangao.
3. Zana ya kufanyia kazi.
1. Chombo cha kutolea mwangaza.
2. Samaki mkubwa mwenye umbo bapa na mkia mrefu.
3. Nidhamu.
1. Sema/eleza.
2. Neno la kukubali jambo.
3. Pengine, labda.
4. Kiwakilishi.
1. Ugonjwa ueneao, au kitu kinachoeneza ugonjwa.
2. Kitu kama gundi kinachonata.
1. Buibui mkubwa.
2. Rafiki.
3. Mchezo wa watoto.
1. Panya mkubwa.
2. kitabu kilichopigwa chapa.
1. Mtaro wenye maji yanayotiririka wakati wote.
2. Mfuko ulio na pamba wa kuegemezea kichwa. Huingizwa kwenye foronya. Mara nyingi huwekwa kitini au kitandani.
1. Uwazi wa kuingilia k.v. nyumba.
2. Familia. -sehemu ya kitabu, sura.
1. Aina ya pambo.
2. Kidudu cha baharini chenye sumu.
3. Mtu anayefanya mambo ya kuchekesha.
4. Aina ya samaki wa baharini.
1. Kitu kisichokomaa, -enye umri mdogo.
2. Toa kitu k.v. fedha ili kukusanya kwa lengo fulani.
1. Mithili.
2. Bana/kaba.
1. Eropleni.
2. Nyuni.
1. Mtoto wa nyuki.
2. Siku kabla ya leo.
1. Isiyojaa, kwa mfano; Debe shinda haikosi kutika.
2. Kaa mahali kutwa nzima, au kukuwa katika hali fulani kwa kipindi cha siku nzima.
3. Fanikiwa katika jambo. Pia fuzu.
4. Kuchukuwa nafasi ya kwanza katika mashindano.
5. Kulemea, kuteka na kushinda kitu/mtu/jambo kwa nguvu au uwezo. Pia kuweza.
Mfano: Kwa kuwa Simba alimshinda Sungura kwa nguvu, alimkamata na kumrarua vipande vipande.