Wafanyakazi |
---|
Maswali kadirifu |
- Kunazo kazi aina nyingi duniani.
- Nyingine zinahitaji ujuzi, elimu na tajriba ya kiwango cha juu ukilinganisha na nyingine.
- Maneno hasa ya wafanyakazi hupatikana katika ngeli ya A-WA.
Kwa mfano:- Daktari anafanya upasuaji.
N/B Kwa kila neno, jaribu kutunga sentensi sahihi.
Mifano
1. Mhasibu: Mtaalamu wa kuweka hesabu za fedha. 'Accountant'.
2. Mhandisi/injinia: Mjuzi wa kutengeneza, kuhudumia na kuunda mitambo. 'Engineer'.
3. Tarishi/Katikiro: Anayehudumu ofisini kwa kutumwa kupeleka habari au ujumbe. 'Office messenger'.
4. Bawabu: Mlinzi wa mlangoni. Pia gadi au mlinzi. 'Watchman'.
5. Topasi/chura: Asafishaye choo. Topasi pia ni mtu ambaye hufagia njia na kusanya taka. 'Latrine cleaner'.
6. Tabibu/daktari/mganga: Mwenye ujuzi wa kutibu. 'Physician'.
7. Muuguzi/mualisaji: Ahudumiaye wawele/wagonjwa. 'Nurse'.
8. Msarifu: Anayesimamia na kuidhinisha matumizi mazuri ya fedha katika shirika.
9. Dereva: Aendeshaye vyombo vya nchi kavu k.v. gari. 'Driver'.
10. Nahodha: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya majini k.v. meli. 'Captain'.
11. Rubani: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya angani k.v. ndege. 'Pilot'.
12. Utingo/taniboi: Mpakiaji na mpakuaji wa mizigo kama vile katika gari. Pia mpigadebe 'Conductor or driver assistant'.
13. Hamali/mpagazi/mchukuzi: Abebaye mizigo kwa malipo. 'Carrier'.
14. Machinga: Auzaye bidhaa rejareja kwa kuzungukazunguka. 'Hawker or street trader'.
15. Malenga: Mtunzi stadi wa mashairi na nyimbo. 'Poet'.
16. Manju: Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma. 'Song leader'.
.
17. Kuli: Apakiaye na kupakua shehena za forodhani. 'Dockworker'.
.
18. Dobi: Afuaye na kupiga nguo za watu pasi kwa malipo. 'Laundress(female), or laundryman'.
.
19. Sogora:-
- Fundi wa jambo fulani katika kusema na kutenda.
- Pia fundi wa kupiga ngoma.
.
20. Saisi: Atunzaye wanyama wanaopandwa k.v. punda na farasi.
.
21. Msajili: Awekaye orodha ya kazi, vitu au viumbe. 'Registrar'.
22. Mkalimani/mtarijumani: Afasiriaye lugha moja hadi nyingine. 'Translater'.
23. Sonara: Atengenezaye mapambo kwa kutumia madini. 'Jeweler'.
24. Kinyozi: Anyoaye nywele. 'Barber'.
25. Msusi/msosi: Asukaye watu nywele. 'Braider'.
26. Ngariba: Apashaye wavulana tohara katika jando. 'Professional circumciser'.
27. Mkunga: Awasaidiaye wajawazito kujifungua. 'Midwife'.
28. Kungwi: Afundishaye mwari wa kike au kiume.
29. Mhariri: Asomaye, kusahihisha na kusarifu makala, magazeti n.k. 'Mhariri'.
30. Mshenga: Atumwaye kupeleka habari za ndoa (posa). 'Messenger, confidant, go-between, mathmaker'.
31. Refa: Mwamuzi katika mchezo k.v. soka. 'Referee'.
32. Kasisi: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kikristo. 'Reverend'.
33. Imamu: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kiislamu.
34. Hakimu: Aamuaye kesi katika mahakama. 'Judge'.
Mfano katika sentensi:- Jopo la mahakimu liliketi kuishughulikia kesi hiyo.
35. Kadhi: Hakimu wa kiislamu. 'Muslim judge'.
36. Mlariba: Akopeshaye wengine pesa. 'Moneylender'.
37. Mwekezaji: Anayeweka mali au pesa katika mradi au biashara, kwa ajili ya kupata faida. 'An investor'.
38. Meneja: Msimamizi au kiongozi katika kampuni au shirika. 'Manager'.
39. Karani: Afanyaye kazi ya kuandika k.m. barua na majarida. 'Secretary'.
40. Kocha: Mwalimu wa mchezo k.v. soka. 'Coach, trainer'.
41. Mkutubi: Ahifadhiye vitabu maktabani na kuviazimisha. 'Librarian'.
42. Mnajimu: Mwenye elimu ya nyota. Hutabiri mambo. 'Astrologer'.
43. Mpigaramli: Abashiriaye kwa kupiga bao. 'Fortune teller'.
44. Mwajiri: Aandikaye mtu kwa kazi ya malipo au mshahara. 'Employer'.
45. Mzegazega: Achotaye maji na kuyauza.
46. Dalali: Auzaye bidhaa katika mnada (soko la kushindania bei). 'Auctioneer'.
47. Manamba: Mfanyikazi wa muda katika shamba kubwa.
48. Mnyapara: Msimamizi wa kazi. 'Head, leader'.
49. Mhazili/Sekretari - Atunzaye barua na majarida na kuandika kwa mashine ofisini. 'Secretary'.
50. Mhadhiri: Mwalimu katika chuo kikuu. 'Lecturer'.
51. Mwashi: Ajengaye nyumba kwa mawe. 'Mason'.
52. Mhunzi: Afuaye vitu vya madini ya chuma au bati.
53. Seremala : Atengenezaye samani za mbao au miti. 'Carpenter'.
54. Mfinyanzi: Atengenezaye vyombo vya udongo k.m. vyungu. 'Potter'.
55. Mvuvi: Afanyaye kazi ya kuvua samaki. 'Fisherman'.
56. Mwanaanga: Afanyaye utafiti wa hali ya anga.
57. Mkabidhi: Mtu atunzaye mali kwa ajili ya mwengine.
58. Diwani: Anayewakilisha watu wake katika serikali za wilaya.
59. Mzoataka: Anayeokota, kuzoa au kukusanya taka. 'Garbage collector.'
60. Kaimu: Anayeshikilia cheo au wadhifa fulani kwa muda. 'Deputy, vice, acting etc.'.
Pia, tazama 'Makamu'.
61. Mchongaji - mtu anayechonga miti/mbao, mawe kutengenezea sanamu. 'Sculptor'.