Mahali mbalimbali |
---|
Maswali kadirifu |
- Kuna mahali au sehemu mbalimbali za kufanyia shughuli mbali mbali.
- Yatazame maelezo ya mahali yafuatayo.
1. Maktaba: sehemu ya kuwekea vitabu kwa ajili ya kusoma na kuazima.
2. Makavazi: mahali ambapo vitu vya kale huwekwa kuchunguzwa na kuonyeshwa.
3. Maabara: sehemu ya kufanyia utafiti wa kisayansi.
4. Bohari: sehemu ya kuhifadhia silaha.
5. Karakana: mahali pa kutengenezea vitu kwa mitambo.
6. Hospitalini: sehemu ya kutolea matibabu kwa wagonjwa.
7. Ufuoni/makafani: Sehemu ya kuhifadhia maiti.
8. Pambajio: sehemu katika nyumba ambapo watu hukaa kungojea zamu zao.
9. Sebule: chumba cha kupokelea wageni na cha mazungumzo
10. Hamamuni: chumba cha kuogea.
11. Mahakamani: Mahali ambapo kesi husikilizwa na kuamuliwa.
12. Stanini: Mahali pa kuabiria na kushikia magari ya usafiri ya umma.
13. Kivukomilia: Mahali rasmi pa kuvukia barabarani palipochorwa mistari mieupe.
14. Maegesho: Mahali speshieli pa kuwekea/kuegesha magari.
15. Korokoroni: Chumba katika kituo cha polisi cha kuwafungia washukiwa.
16. Gerezani/Husuni: Sehemu ya kufungiwa wahalifu ili kuadhibiwa warekebishe mienendo yao.
17. Rumande: Chumba katika gereaza wanapofungiwa mahabusu wanaosubiri kumalizika kwa kesi zao.
18. Maabadini: Mahali a kuabudia.
19. Mskitini: maabadi ya waislamu.
20. Hekaluni: Maabadi ya wayahudi.
21. Sinagogi: maabadi ya Wayahudi.
22. Kanisa: maabadi ya Wakristo
23. Mahame: mahali palipohamwa (ganjo/tongo)
24. Kizimbani: sehemu ya mahakamani asimamapo mshtaki, mshtakiwa au shahidi wakati wa kesi.
25. Fuko: mahali kuku hutagia
26. Ghala/stoo: jengo la kuhifadhia bidhaa
27. Madobini fuo: mahali maalum ambapo madobi hufulia nguo
28. Chimbo: shimo kubwa ambapo huchimbuliwa udongo, mchanga au madini.
29. Mapokezi: ofisi ya kupokelea wageni
30. Kilinge: mahali pa uganga