Mahali mbalimbali |
---|
Maswali kadirifu |
1. Chumba cha kufanyia utafiti wa kisayansi ni ____________.
2. Chumba cha wanafunzi cha kulia huitwa ______________.
3. Mahali pa kuokea vyungu huitwa ____________.
4. Sehemu ya kuhifadhi nafaka ni __________.
5. Nyumba ya kujilindia kutokana na adui huitwa _________.
6. Ukumbi wa mazungumzo huitwa _________.
7. Mahali k.v meza pa kutolea huduma mbalimbali huitwa _________.
8. Mahali pa kushuka pwani kutoka melini huitwa ____________.
9. Mahali panapouzwa chai: kahawa na vyakula vingine huitwa ______.
10. Mahali pa kutengenezea vyombo vya usafiri huitwa _________.
11. Chumba cha kupigia na kurushia picha huitwaje? __________.
12. Wanyama hupelekwa __________ kula.
13. Mahali ambapo wanyama huchinjiwa huitwa _______________.
14. Sehemu ambapo mtu huenda haja ni ________________.
15. Mahali ambapo wavulana hutahiriwa huitwaje? ___________
16. Mahali panapouzwa chakula na vinywaji k.v katika shule huitwa ____________.
17. Duka la vipodozi na utengenezaji wa nywele huitwa _______________.
18. Mahali pa kuogeshea mifugo k.v. mbuzi na ng’ombe huitwaje? ______________.
19. Nyumba ya kulala wanafunzi katika shule au chuo huitwa _____________.
20. Mahali pa kupikia ni _______________.