Maumbile ya nchi
Maumbile ya nchi ni kama vile:
- Mto: Bonde lenye maji yanayotiririka wakati wote.
- Ziwa: Sehemu yenye maji mengi iliyozungukwa na nchi kavu.
- Bahari: Eneo kubwa la maji ya chumvi linalozungukwa na nchi kavu.
- Upwa: Sehemu ya pwani ambayo maji hujaa na hupwa.
- Delta: Sehemu mto unapojigawaganya vipande viwili au zaidi unapoingia baharini.
- Kinamasi: Mahali penye tope au telezi.
- Chemchemi: Mahali maji yanapobubujika.
- Gema/genge/korongo: mteremko mkali kwenye kingo za mto.
- Kisiwa: Eneo la nchi kavu lililozungukwa na maji.
- Msitu: Eneo kubwa lililo na miti mingi.
- Nyika: Sehemu inayoota nyasi na miti midogo.
- Jangwa: Eneo kubwa na kame ambalo kwa kawaida huwa na mchanga lisiloota nyasi wala miti.
- Tambarare: Nchi isiyokuwa na miinuko wala mabonde.
- Bonde: Sehemu ya ardhi iliyo katikati ya vilima viwili.
- Mlima: Sehemu ya ardhi iliyoinuka juu sana kuliko sehemu nyingine.
- Nguu: Sehemu ya juu kabisa ya mlima.
- Volkano: Mlipuko mkali wa moto unaotokea ndani ya dunia kumwaga zaha ambayo mara nyingi husababisha milima katika uso wa dunia.
- Kreta: Sehemu inayopatikana juu ya mlima. kifungulima:
- Kisima cha jangwani. Kisiwa: Eneo la nchi kavu lililozungukwa na maji.
- Wangwa: Sehemu ya pwani iliyo na mikoko ambapo maji hujaa na kupwa.
- Ghuba: Sehemu kubwa ya bahari iliyoingia ndani ya pwani.
- Mgodi: Mahali palipochimbuliwa madini.
- Kituka: Mahali penye miti mifupimifupi iliyoshonana na nyasi.