Utangulizi |
---|
Mifugo |
Wanyamapori |
Viumbe vya majini |
Ndege/Nyuni |
Maswali kadirifu |
Mifano ya wanyamapori
1. Simba - Ni mnyama wa jamii ya paka, lakini mkubwa na mwenye rangi ya hudhurungi au majani makavu mwili mzima na alaye nyama.
2. Ndovu/tembo - Ni mnyama wa porini aliye mkubwa sana, mwenye masikio makubwa na mapana, mkonga ambao huutumia kukata majani ya kula, huchota maji na pembe mbili ambazo zina dhamana kubwa na mara nyingi huwindwa na majangili kwa sababu ya pembe zake.
3. Chui - Mnyama anayekula nyama ambaye anafanana na paka, mkubwa na mwenye kasi sana na hupatikana Asia na Afrika.
4. Duma - Ni myama anayefanana na chui ambaye ana rangi ya manjano na mabaka meusi.
5. Chui milia -
6. Punda milia - Ni mnyama wa porini anayefanana na farasi au punda na mwenye ngozi yenye miraba meupe na mieusi mwilini.
7. Paa - Ni mnyama wa porini anayefanana na mbuzi.
8. Kifaru - Ni mnyama mkubwa wa porini anayefanana na kiboko mwenye pembe moja juu ya pua.
9. Nyati/mbogo - Ni mnyama wa porini wa jamii ya ngombe lakini mkubwa na mwenye pembe kubwa zilizopinda kuelekea mbele.
10. Simba marara /fisi - Mnyama wa porini mwenye rangi ya kijivu na anayekula mizoga; bakaya (mse).
11. Mbweha - Mnyama wa mwituni mdogo kuliko mbwa mwitu mwenye masikio marefu yaliyosimama na mdomo mrefu.
12. Pofu/mbungu - Mnyama wa jamii ya ng'ombe lakinimwenye kichwa kama cha swara.
13. Swara - Ni mnyama mwitu anayefana na mbuzi.
14. Tohe - Ni mnyama wa porini wa jamii ya paa mwenye pembe fupi sana.
15. Kongoni/ngosi/topi - Ni mnyama anayefanana na ng'ombe anayeishi porini, mwenye miguu ya mbele iliyo mirefu zaidi kuliko ya nyuma, mkia kama wa farasi, manyoya mengi shingoni na kichwa kirefu chenye pembe.
16. Sokwe - Ni mnyama wa jamii ya nyani ambaye ni mkubwa zaidi na hana mkia.
17. Tumbili - Ni mnyama wa jamii ya nyani mwenye rangi ya kijivu isiyokoza, baka jekundu matakoni na mkia mrefu.
18. Twiga - Ni mnyama mrefu sana wa bara la Afrika mwenye rangi ya kahawia na mabatobato mweusi, miguu mirefu na shingo ndefu.
19. Kuro - Ni mnyama wa porini wa jamii ya paa ambaye anafanana na kulungu.
20. Mbango - Ni mnyama mdogo wa porini wa jamii wa nguruwe ambaye meno yake mawili ya mbele yametokeza nje.
21. Kimburu - Ni mnyama pori wa jamii ya paka mwitu apendaye sana kuwakamata ndege hasa kuku.
22. Kingugwa - Mnyama mithili ya fisi mwenye mamdoadoa.
23. Kicheche - Ni mnyama wa jamii ya paka mwitu mwenye mkia mrefu na manyoya mengi anayekula kuku.
24. Kanu - Paka mwitu mwenye mkia mweupe ulio na manyoya mengi mwenye kasi sana na hupenda nyama ya kuku.
25. Mindi - Mnyama pori anayefanana na funo(mnyama wa porini anayefanana na paa)
26. Mbarapi - Mnyama wa jamii ya paa mwenye miguu miembamba.
27. Porapora - Ni mnyama mwenye milia wa jamii ya nyegere alaye nyuki.
28. Nyegere - mnyama mdogo mweusi mwenye kichwa kikubwa na masikio madogo ya mviringo, rangi nyeupe au kijivu mgongoni na anapenda kula asli sana.
28. Komba - Mnyama mdogo ambaye hulala wakati wa mchana na hutenbea na kulialia sana usiku.