Vikembe
- Vikembe pia huitwa vizawa.
- Vikembe ni wana wa viumbe mbalimbali.
Mifano;
- Malaika - Mtoto wa binadamu.
- Ndama - Mtoto wa ng’ombe, ndovu.
- Funutu/maige/kimatu/tunutu - Mtoto wa nzige.
- Jana/chana – Mtoto wa nyuki.
- Kifaranga – Mtoto wa kuku.
- Kinda – mtoto wa ndege/nyuni.
- Kiluwiluwi – Mtoto wa chura, mbu.
- Kiwavi – Mtoto wa kipepeo.
- Kitungulekituju – Mtoto wa sungura.
- Kihongwe – Mtoto wa punda.
- King’onyo – Mtoto wa mdudu.
- Kilebu – Mtoto wa mbwa/kelbu.
- Kigunge - mtoto wa nyami.
- Kivinimbi – Mtoto wa nguruwe.
- Chengo – Mtoto wa nyangumi.
- Kinyaunyau – Mtoto wa paka.
- Kibuli/kimeme – Mtoto wa mbuzi.
- Nyumbu – Mtoto kati ya punda na farasi.
- Chotara/hafukasti/suriama/shombe – mtoto kati ya wazazi wa rangi mbalimbali.
- Saraka/athiari/jarari/dawati – mtoto wa meza.
- Kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu - mtoto wa nzige.
- Kitekli - mtoto wa farasi.
- Kigwena - mtoto wa mamba.
- Kikuto'kisui/chongole - mtoto wa fisi.
- Nirigi/nirihi - mtoto wa ngamia.
- Kidanga - mtoto wa ndovu.
- Nyamawa - mtoto wa mbweha.
- Kibebe/katama - mtoto wa kondoo.
- Kichengo - mtoto wa samaki.
- Kinyemere - mtoto wa nyoka.