Mavazi |
---|
Maswali kadirifu |
- Mavazi huvaliwa mwilini.
- Yapo mavazi ya aina nyingi.
1. Rinda - kanzu ya kike pana iliyokatwa kiunoni.
2. Kikoi - hufungwa kiunoni na kuteremka hadi miguuni.
3. Buibui/baibui - vazi jeusi livaliwalo juu ya nguo nyingine.
4. Ubinda - hupitishwa baina ya mapaja.
5. Saruni - hufungwa kiunoni na kuteremka hadi miguuni.
6. Kibwebwe/mahazamu -hufungwa kiunoni.
7. Masombo -Huviringwa na kufungwa kiunoni.
8. Gagulo - kirinda kidogo.
9. Kanchiri/sidiria - huvaliwa kifuani.
10. Kaniki -kanga ya kujifunga wakati wa kazi.
11. Ukaya - kitambaa cha usoni.
12. Kizibao -koti fupi lisilo na mikono.
13. Blauzi - nguo ifananayo na shati.
14. Kimono -kanzu fupi ya mtindo wa Ujapani.
15. Suti - sketi au suruali pamoja na koti ziliozofanana kwa kitambaa na rangi.
16. Gauni - kanzu yenye marinda.
17. Bombo -kaptura. Suruali fupi iishiayo juu ya magoti au kwenye magoti. Pia huvaliwa na wanawake.
18. Shati -vazi la sehemu ya juu ya mwili lililo na ukosi na mikono.
19. Sweta -fulana nzito ya sufi. Pia huvaliwa na wanawake.
20. Kitenge - Nguo mfano wa kanga.
21. Surupwenye/ovaroli -vazi la juu la kuzuia mavazi mengine yasichafuke wakati wa kazi. Pia huvaliwa na wanawake (bwilasuti)
22. Suruali -vazi la kiunoni hadi kwenye jicho la mguu lenye nafasi mbili za kupenyezea miguu. Pia huvaliwa na wanawake.
23. Joho -koti pana na refu lililo wazi sehemu ya mbele.
24. Kilemba -Kitambaa au nguo inayozungushwa kichwani (pia wanawake huvaa).
1. Kocho (jumla)
2. Sidiria – wanawake
3. Shimizi/kamisi – wanawake
1. Chepeo – kofia kubwa yenye ukingo duara uliotokeza nje (“samahani jua”)
2. Tarbushi/kitunga – kofia yenye shada la nyuzi ndefu.
3. Kidotia – kofia ya mtoto.
4. Bulibuli – kofia nyeupe iliyotiwa nakshi.
5. Boshori – kofia ya mtoto.
1. Njuti, buti
2. Kubadhi
3. Ndara, slipa, lapa
Pia kuna viatu viitavyo mtarawanda.