Mavazi |
---|
Maswali kadirifu |
Viteuzi: buibui, kanchiri, chepeo, tarbushi, kisutu, dangarizi, sare, shimizi.
1. Wanawake wa Kiislamu huvaa vazi jeusi juu ya nguo zaoza kawaida. Vazi hilo huitwa _____.
2. Nguo za wanafunzi shuleni huitwa _____.
3. Vazi linalovaliwa ndani ya rinda na wanawake huitwa _____.
4. Suruali ndefu iliyoshonwa kwa kitambaa kigumu aghalabu cha rangi samawati huitwa ____.
5. Kivazi kinachovaliwa na wanawake vifuani ili kusetiri dodo huitwa _____.
6. Kofia ya 'samahani jua' pia huitwa _____.
7. Kanga ambazo zimetiwa nakshi ya kila aina huitwa _____.
Mfano: sharti - wanaume kocho - wote
blauzi - wanawake ubinda - watoto
1. kaniki 2. gaguro
3. kirinda 4. seruni
5. fulana 6. pajama
7. bwelasuti 8. suruali
9. bombo 10. shimizi
11. mahazamu 12. shali
13. kanzu 14. buibui 15. kikoi