Sayari |
---|
Maswali kadirifu |
Jaza nafasi kikamilifu.
1. Sayari iliyo kubwa zaidi kati ya zote ni ipi?
2. Sayari iliyo na joto zaidi ni ipi?
3. Kulingana na utafiti, ni sayari ipi isipokuwa dunia inayoaminika kuwa binadamu anaweza kuishi?
4. Ni sayari ipi iliyo na baridi zaidi?
5. Sayari ipi inayoaminika kuwa na miezi mingi zaidi?
6. Taja sayari mbili zilizopakana na dunia.
(i) ___________ (ii) ___________.
7. Ni sayari ipi ndogo kuliko zote tisa?
8. Ni sayari ipi iliyo katikati ya zote?
9. Ni sayari ipi jirani ya utaridi?
10. Taja sayari tatu zinazoyachukua masafa marefu zaidi kulizunguka jua.
Toa jibu bora.
1. Sayari hung'aa nazo nyota _____.
2. Elimu ya nyota huitwa _____.
3. Jua pamoja na sayari zote huitwa mfumo wa _____.
4. _____ ni sayari ndogo kuliko zote.
5. _____ ni sayari kubwa kuliko zote.
6. _____ hujulikana kama nyota ya alfajiri.
7. ____ ni sayari ambayo haina mwezi.
8. Sayari yeny peteo huitwa _____.
9. Sayari iliyo mbali kabisa huitwaje?_____.
10. Mbalamwezi _____ .( humeta au hung'ara)
11. Tega vitendawili ambavyo viteguzi vyake ni : a) Jua b) mwezi c) nyota
12. Chora mfumo wa jua na sayari zote.