Ala za muziki |
---|
Maswali kadirifu |
Ala za muziki ni vyombo vya kuchezea muziki.
1. Ngoma: Ala ya muziki ambayo hutengenezwa kwa kuamba ngozi k.v. ya ng’ombe kwenye mzinga.
2. Tarumbeta: Ala ya muziki ya kupulizia ambayo vali zake hubonyezwa ili kubadilisha sauti.
3. Kinubi: Zeze ambalo lina nyuzi na hupigwa huku limesimamishwa.
4. Harimuni/kodiani: Kinanda ambacho hutoa sauti, kwa kubonyeza na kuvuta kwa mikono.
5. Manyanga: Chombo kilichowekwa vijiwe vidogovidogo kinachotumika kama ala ya muziki.
6. Njuga/msewe: Kengele ndogo zifungwazo shingoni, mkononi na hata miguuni wakati wa kucheza ngoma.
7. Saksafoni: Ala ya muziki ya kupuliza ambayo hubadilishwa sauti kwa kubonyeza vifungo vyake.
8. Mbiu: Pembe ya mnyama inayopulizwa wakati wa kucheza ngoma.
9. Gitaa/gita: Ala ya muziki ambayo hupigwa kwa vidole. Kwa kawaida, huwa na nyuzi sita.
10. Buruji: Tarumbeta ndogo.
11. Kayamba: Chombo chenye changarawe ndani na hutikiswa wakati wa kuimba.
12. Piano: Chombo cha muziki kilicho na vibanzi vinavyobonyezwa na kutoa sauti.
13. Fidla: Ala ya muziki mfano wa gita ndogo.
14. Filimbi: Chombo kitoacho sauti kinapopulizwa.
15. Marimba: Ala ya muziki mfano wa sanduku hutengenezwa kwa mbao na vibao vyembemba hutandikwa. Vipigwapo kwa virungu viwili hutoa sauti.
16. Zeze: Ala ambayo ina nyuzi kama za gita.
17. Tari/dafu: Ngoma ndogo iliyoambwa upande mmoja na kuwekwa vibati kwenye kingo zake.
18. Nai: Ni ala iliyo na umbo la filimbi ingawa haina tundu nyingi.
19. Baragumu: Pembe kubwa iliyotobolewa shimo ndogo karibu na ncha yake.
20. Zumari/Nzumari: Ala ya muzik iambayo ni nyembamba mdomoni na pana upande unakotokea sauti. Tundu hutoa sauti mbalimbali.
21. Upatu: Chombo chenye umbo la sinia, cha chuma kipigwacho na kutoa sauti.
22. Gambusi: Ala ya muziki ifananayo na banjo.
23. Msondo: Ngoma ndefu na kubwa.
24. Chapuo: Ngoma ndogo iliyowambwa pande zote mbili.
25. Udi: Ala ya muziki inayofanana na gita bali ni pana upande.
26. Banjo: Ala ya muziki iliyo na nyaya nne au zaidi. Ina shingo ndefu na kitako kipana.
27. Kuro: Ngoma kubwa inayosimama kwa miguu mitatu.