Biashara |
---|
Maswahili kadirifu |
- Biashara inahusu ununuzi na uuzaji wa bidhaa na/au huduma.
- Mifano ya bidhaa ni kama vile nguo, magari, chakula n.k.
- Mifano ya huduma ni kama vile bima, simu n.k.
- Kwa kawaida lengo la msingi la kufanya/kupiga biashara ni kupata faida ingawa mara kwa mara, hasara hupatikana.
- Biashara inaweza kuwa ya kitaifa (hufanywa katika taifa moja) na pia ya kimataifa (hufanywa baina ya mataifa zaidi ya moja).
1. Faida/tijara/kivuno/chumo/ziada - Pato libakialo baada ya kuondoa gharama za kufanya biashara k.v. ununuzi na usafirishaji.
2. Hasara -Ukosefu wa faida; Hali ya kupoteza pato au mali katika biashara.
3. Bei -Kiwango cha pesa kununulia au kuuzia bidhaa au huduma fulani.
4. Uuzaji wa rejareja -Uuzaji wa kiasi kidogo kidogo.
5. Uuzaji wa jumla - Uuzaji wa kwa pamoja.
6. a) Bei rafi - Bei ambayo haipunguzwi.
b) Kipimo rafi - Kipimo ambacho hakipunguzwi.
c) Bei ya kuruka - Bei isiyokubalika kisheria/haramu.
7. Raslimali - Ujumla wa mali yaanyomilikiwa na mtu au nchi.
8. Malighafi -Mali yanayotumika kutengeneza vitu vingine k.m. pamba ni malighafi ya kutengenezea nguo.
9. Maliasili -Utajiri kama vile madini, misitu, maziwa, mito, anga vinavyopatikana katika mazingira.
10. Uwekezaji - Kutumia pesa/mali ili kuzalisha fedha/mali zaidi.(ilikupata faida).
11. Kitegauchumi - Rasilmali k.v. kiwanda inayotumika kuzalisha mali.
12. Ujasiriamali -Uwekezaji mtaji katika biashara.
13. Mtaji -Mali ya kuanzisha biashara au kuipanulia.
14. Ulanguzi -Ufichaji wa bidhaa ili bei yazo iruke.
15. Magendo -Upigaji biashara kwa njia haramu/isiyo halali.
16. Chenji -Pesa zinazobaki baada ya kununua kitu.
17. Maduhuli - Bidhaa ambazo hununuliwa kutoka nchi za nje.
18. Mahuruji - Bidhaa zinazouzwa nchi za nje.
19. Ushuru - Kodi ya kuingiza bidhaa nchini au kuziuza/Ada ya forodha.
20. Ruzuku - Pesa zinazotolewa na serikali kwa idara mbalimbali ili kujiendeleza.
21. Mshtiri - Mnunuzi.
22. Mteja - Aendaye kununua bidhaa au huduma.
23. Wakala - Ajenti.
24. Utandawazi -Utaratibu wa mataifa kushirikiana katika nyanja mbalimbali k.v. biashara.
25. Ubinafsishaji -Hali ya kusababisha mali ya umma imilikiwe na watu binafsi.
26. Ubia -Ushirikiano wa watu wawili au zaidi katika shughuli k.v. ya biashara.
27. Hawala - Hundi/cheki.
28. Amana - Kitu unachomwekea mwenzako hadi atakapokihitaji.
29. Turuhani/kipunguzo – Kiwango kinachotolewa kutoka katika bei iliyotangazwa.
30. Ikfisadi -Uangalifu katika kutumia fedha/mali.
31. Ubepari -Mfumo wa uchumi ambao unawawezesha watu wachache kumiliki raslimali na vitegauchumi.
32. Ukiritimba -Hali ya kuzuia wengine kufanya biashara au kushindana katika biashara.
33. Dukakuu - Duka kubwa ambapo wateja hujichukulia bidhaa watakazo kutoka rafuni.
34. Hisa - Sehemu ya mtaji katika biashara.