Maeneo ya utawala
- Katika taifa k.v. Kenya, utawala au uongozi huwekwa katika ngazi mbalimbali.
- Tukianzia chini, muundo wa utawala huwa hivi:
- Kata ndogo – huongozwa na naibu wa chifu.
- Kata/lokesheni – huongozwa na chifu.
- Tarafa/divisheni – huongozwa na mkuu wa tarafa.
- Wilaya/mudiria – huongozwa na mudiri.
- Mkoa – huongozwa na mkuu wa mkoa (pisii).
- Taifa – huongozwa na raisi.