Vimelea |
---|
Maswali kadirifu |
- Vimelea ni mimea au wadudu wanaoishi kwa kuvitegemea viumbe au mimea mingine.
- Tafsiri ya vimelea kwa kiingereza ni 'Parasites'.
- Katika binadamu, tuna vimelea wa nje na wengine hukaa ndani ya mwili wa binadamu.
- Inamaanisha kuwa kuna vimelea wanaoathiri wanadamu na wale wanaoathiri wanyama.
1. Kiroboto – mdudu aumaye, hukaa mavazini au manyoyani.
2. Kitumbi – funza apenyaye ngozi ya mtu na kukaa huko.
3. Chawa – mdudu akaaye mwilini mwa mwanadamu, nguo chafu na nywele chafu.
4. Kunguni – mdudu afyonzaye damu na hukaa vitandani, pongoni, vitini n.k.
5. Funza/tekenya/bombwe – mdudu akaaye kwenye miguu ya watu.
6. Mbung’o/ndorobo/chafuo/pange– mdudu kama nzi na aumaye na kusababisha malale.
7. Mbu – mdudu afyonzaye damu na kusababisha malaria.
8. Papasi – mdudu mweupe afananaye na kunguni na huuma. Huleta homa ya vipindi kwa binadamu.