Viungo vya mwili |
---|
Maswali kadirifu |
Miguu, kisogo, pua, kiganja, shingo, sikio, kinywa, mgongo, mkono, kichwa, viganja, nyonga, nywele, kidevu
1. ___________ ya kuitikiza sio uchungu.
2. ___________ hubeba vyombo, roho hubeba mambo.
3. ___________ kamwambia ndevu kila mtu apataye huwa mwerevu.
4. ___________ jumba la maneno.
5. Masikio hayapiti ___________
6. ___________ la kufa halisikii dawa.
7. Kofi hazilii ila kwa ___________
8. Mpa ___________ si mwenzio.
9. ___________ hayana pazia.
10. Mpiga ngumi ukuta huumiza ___________ wake.
11 ___________ mtupu haurambwi.
12. Vita havina ___________.
13. ___________ mmoja haubebi mwana.
14. Mwana hutazama _________ cha nina.
15. Akimbiaye huagana na ____________.
16. ________________ ni shajara.
17. Akili ni______________ kila mtu ana zake.
18. ___________ alichonyia mwana huoshwa hakitatwi.
19. Mtembezi hula ___________ yake.
20. Kata ___________ uunge wajihi.