Maswali kadirifu

A. Jaza mapengo

1. Mahali ambapo kesi huamuliwa huitwa _____.

2. Kukata rufani ni kufanya nini?_____.

3. Hakimu wa mahakama za kislamu huitwa _____.

4. Anayetoa uamuxi wa kesi mahakamani za Kiislamu huitwa ____.

5. Kesi ya jinai ni gani?

6. Nini maana ya mahabusu?

7. Daawa ni kesi sampuli gani ?

8.Anayeongoza mashtakaa kortini huitwa _____.

9. Washukiwa mara nyingi huachiliwa kwa _____ wakati kesi inapokuwa ikiendelea.

10.  _____ ni uamuzi katika kesi.

11. Shahidi ni nani?

12. Shahidi husimama wapi anapotoa ushahidi mahakamani?

13. Uamuzi wa kimahakama huitwaje? _____.

14. Kisawe cha mahakamai ni _______.

15. Tofautisha hatia na dhambi.

 

B. Toa maelezo kuhusu:

  1. faini au fidia
  2. hakimu
  3. karani wa kortini
  4. mlalamishi
  5. mshukiwa au mtuhumiwa
  6. mahakama kuu
  7. mahakama ya rufaa
  8. kiri mashtaka
  9. pingu
  10. kifungo

C. Jibu maswali yafuatayo ukitumia msamiati sahihi wa korti uliopewa hapa.

kiongozi wa mashtaka, husuni, kizimbani, dhamana, ithibati, wakili, rumande; shahidi, faini, korokoro.

 

1.Katika kesi hiyo, askari walileta pombe haramu iliyonaswa kama _____.

2. Mshtakiwa alipopatwa na hatia, alihukumiwa kutoa ______ ya shilingi elfu tano.

3. Licha ya kutetewa na ______ wake, mshtakiwa hakuepuka kifungo gerezani.

4. Ilimbidi mshukiwa apelekwe rumande aliposhindwa kulipa _____.

5. Mshtakiwa alitulia pale _________ alipoyasikiliza mashtaka yakisomwa.

6. Atoaye ushahidi mahakamani huitwa ________.

7. _____________ huongoza mashtaka dhidi ya mshukiwa.

8. Chumba cha kufungia mshukiwa katika kituo cha polisi ni ______.

9. Mahabusu hutumikia kifungo chake katika _________

10. Mshtakiwa alipokataa mashtaka, aliamriwa arudishwe ____ kwa wiki mbili.