Michezo

- Michezo ni jambo linalofanywa na watu washindanao/washindani.

- Aidha, michezo inaweza kufanywa kwa ajili ya kujifurahisha.

Aina za michezo

1. Soka/kandanda/kambumbu - mchezo unaochzwa kwa miguu wenye timu mbili zinazoshindana.           

2. Miereka 

3. Mpira wa vikapu  

4. Voliboli - mchezo wa timu ya watu sita unaochezwa kwa mikono kwa kupiga mpira na kuuvusha juu ya wavu ulioweka katikati ya kiwanja kuelekea timu pinzani.

5. Mpira wa pete/netiboli - mchezo wa mpira wa mikono unaochezwa na watu saba kila upande kwenye uwanja ambao goli zake ni milingoti miwili mirefu yenye pete na nyavu.

6. Hoki- mchezo wa mpira ambao wachezaji hucheza kwa kutumia magongo maalumu.

7. Gofu - mchezo unaochezwa kwa kuupiga mpira mdogo kwa kingoe.

8. Naga/gori - mchezo unaofanana na mpira wa mguu ambao wachezaji huruhusiwa kukamata mpira na kukimbia nao.

9. Chesi/saratanji/bao - mchezo unaofanana na bao ambao  huchezwa na watu wawili ambapo kila mmoja anakuwa na vipande 6 vya kucheza vinavyoweza kusogezwa juu ya ubao wenye umbo mraba kwa uelekeo tofauti.

10. Kareti - mtindo wa upiganaji wa kijapani ambapo mpiganaji hutumia mikono na miguu.

 

11. Judo - mchezo wa mieleka ambao huchezwa na watu wawiliwawili.

12. Kriketi - mchezo unaochezwa na timu mbili ambapo kila moja inakuwa na mchezaji.

13. Kuruka kwa upondo

14. Kuruka juu

 15. Kuruka urefu

16. Mbio - mwendo wa kasi au upesi.

17. Kuruka viunzi

18. Magongo

19. Jugwe - mchezo wa kuvutana kwa kamba unaochezwana timu mbili zenye wachezaji kumi na wawili kila moja.

20. Msabaka - mashindano ya mbio za farasi wanaoongozwa na wapanda farasi.

 

21. Sarakasi - michezo inayofanywa kwa ustadi mkubwa ambayo huonyesha matendo ya kishujaa na ya kushangaza.

22. Mlenge - mashidano ya kulenga shabaha kwa kutupa vijiti vunane.

23. Taekwondo

24. Kuruka kamba

25. Kuteleza barafuni

26. Mbio za magari

27. Mbio za pikipiki

28. Mbio za baiskeli

29. Langalanga

30. Kuogelea

Michezo mbalimbali.

[resource: 7932, align: left]