Hospitalini |
---|
Maswali kadirifu |
- Hospitalini ni mahali pa kutibia wawele.
- Kunazo hospitali kubwa na nyingine ndogo. Hospitali ndogo huitwa dispensari au zahanati.
1. Pambajio - Sehemu ya kuwapokelea wagonjwa.
2. Wodi - Sehemu ya kuwalaza wagonjwa wanapoendelea kupokea matibabu.
3. Kungawi – chumba cha kujifungulia wajawazito.
4. Chumba cha upasuaji – chumba cha kufanyiwa upasuaji wa wagonjwa.
5. Wodi ya matibabu maalum – Chumba cha kushughulikia maradhi ambayo si ya kawaida k.m. maradhi ambayo yamezuka ghafla na bado hayaeleweki vizuri.
6. Chumba cha matibabu ya dharura – chumba cha kuwatibia wale wanaohitaji matibabu ya haraka sana k.m. wahasiriwa wa ajali.
7. Chumba cha matibabu ya kina – chumba cha matibabu ya kiwango cha juu sana. Hususan hutumiwa kwa wale walio katika hali mahututi. Chumba hiki huwa na mitambo na mashine za hali ya juu sana za kumsaidia mgonjwa.
8. Maabara – chumba cha kufanyia utafiti.
9. Chumba cha dawa – Chumba cha kuhifadhia dawa zitolewazo kwa wagonjwa.
10. Ufuoni/makafani – mahali pa kuhifadhia maiti.
1. Eksrei / uyoka – mashine ya kuonea viungo vya ndani ya mwili.
2. Machela – kigari au kitanda cha kubebea wagonjwa.
3. Mikroskopu/hadubini – kifaa kitumiwacho kuangalia vitu vidogo.
4. Dipriza – chombo cha kuhifadhia baadhi za dawa zinazohitaji kuhifadhiwa katika kiwango cha baridi sana.
5. Jiko – chombo cha kuchemshia vyombo ili kuulia viini na bakteria.
6. Glovu – kitu kama soksi kitengenezwacho kwa mpira na huwekwa mkononi kukingia uchafu.
7. Sindano – kifaa cha kupenyezea dawa mwilini.
8. Sirinji – mfereji mdogo wa kutilia dawa kwa ajili ya kudungia sindano na kutolea dawa.
9. Makasi – kifaa ambacho hutumiwa kwa kukatia.
10. Bendeji – kitambaa cha kufungia jeraha au kidonda.
11. Plasta – kitambaa kigumu sana cha kufungia sehemu iliyovunjika
12. Koleo – Kifaa cha kushikia vitu vinavyotumika na daktari
- Ugonjwa ni hali au kitu kinachomfanya mtu, mnyama au mmea kuwa katika afya/siha duni.
- Kunayo maradhi chungu nzima yanayoweza kumwathiri mja.
- Mengine yanatiba mengine hayana.
- Mengine yanaambukiza.
- Maradhi ya kuambukiza ni yale yanayoenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.
Saratani/kansa: ugonjwa usio na tiba kwa sasa. Ni ukuaji usio wa kawaida wa seli katika mwili.
Malale: ugonjwa wa usingizi unaoambukizwa na mbung’o.
Homa ya matumbo: taifodi
Kwashakoo/ukosandisha: uele wa watoto unaosababishwa na uhaba wa chakula hususan protini.
Surua/shurua/firangi/ukambi: ugonjwa wa watoto unaofanya ngozi kuwa na vipele. Hatua za kwanza huwa ni homa kali.
Mafua/bombo: maradhi ya kuambukiza yanayosababisha mgonjwa kuumwa na koo na kichwa. Mgonjwa hutokwa na kamasi na kuwa na homa.
Kaputula: uele wa kuhara. Tumbo la kuendesha.
Baridi yabisi: maumivu ya mifupa au viungo yanayosababishwa na baridi shadidi.
Ukoma: uele wa kuambukiza wa mabatomabato ambao unaharibu mishipa ya fahamu na kukata viungo vya mwili.
Matumbwitumbwi/machibwichibwi: ugonjwa wa kuvimba mashavu hadi chini ya taya hususan kwa watoto
Kisunzi/kizunguzungu/masua/gumbizi: uele wa kuhisi kichwa kikizunguka.
Kipwepwe: ugonjwa wa ngozi unaosababisha madoa mekundu unaodaiwa kuletwa na chawa.
Ndui: ugonjwa unaosababisha pele nyingi zenye majimaji na usaha.
Kororo: uele wa kuvimba kooni.
Ngiri: ugonjwa wa kukazana kwa mishipa iliyo sehemu za chini ya kitovu.
Zongo: ugonjwa wa kuvimba tumbo kwa watoto wadogo.
Vimbizi: hali ya kutoweza kupata pumzi kutokana na chakula kutosagika tumboni.
Mbalanga/barasi: uwele unaobadilisha rangi ya ngozi na kuwa na mabaka au matone.
Rovu: ugonjwa wa kuvimba tezi kwenye shingo.
Tetekuwanga/galagala/tetemaji: ugonjwa wa pele na homa kali wa kuambukizwa sanasana kwa watoto.
1. Daktari/tabibu – anayewatibu wagonjwa.
2. Muuguzi/nesi – anayemsaidia daktari kuwatibu wagonjwa.
3. Mkunga – anayewasaidia wajawazito kujifungua.
4. Mhazigi – Anayeshughulikia waliovunjika viungo.
5. Msaidizi katika maabara – anayewahudumia wagonjwa katika maabara.
6. Karani – huweka rekodi za wagonjwa.
7. Mfamasia – anayeweka na kuzitoa dawa kwa wagonjwa.
8. Daktari wa meno – hushughulikia wagonjwa walio na matatizo ya meno.