Alama za barabarani |
---|
Maswali kadirifu |
- Alama za barabarani zina umuhimu mkubwa mno. Zinatoa maelekezo na pia kuonya.
- Upuuzaji wa alama za barabarani mara kwa mara husababisha ajali za barabarani.
- Ni muhali basi sisi sote kuzitilia maanani alama hizo.
1. Taa za barabarani:
Rangi nyekundu (red)– dereva asimamishe gari.
Rangi ya kaharabu (amber) – dereva awe tayari kuondoka.
Rangi ya kijani (green)– dereva aondoke iwapo njia ni wazi.
- Mtembeaji anastahili kuvuka barabara aonapo rangi ya kijani.
Hata hivyo, sharti ahakikishe barabara ni wazi yaani haina magari.
2. Kivukomilia (zebra crossing) – sehemu iliyochorwa mistari mieupe na ndiyo rasmi ya kuvukia barabara, kwa wale wanaotembea kwa miguu.
3. Simama
4. Hakuna njia ya kuingia - No entry.
5. Baiskeli zisitumike.
6. Watembeaji kwa miguu wamekatazwa.
7. Hakuna kugeuka upande wa kulia.
8. Hakuna kugeuka upande wa kushoto. Alama hizi mbili hupatikana katika njia panda.
10. Usiegeshe gari lako.
9. Usilipite gari jingine.
11. Usiendeshe kwa kasi iliyozidi ulivyoonyeshwa.
12. Mbele pana kuruba ya kushoto.
13. Mbele pana kuruba ya kulia.
14. Pana matuta ya barabarani.
15. Mzunguko wa barabarani.
16. Watoto wanaweza kuwa wakipita.
17. Waendeshaji baiskeli wanaweza kupatikana.
18. Ng’ombe wanaweza kuwa wakipita.
19. Pana hatari fulani mbele.
20. Kuna kazi inayoendelea barabarani.
1. Kuruba - (A bend or a turn).
2. Tuta | matuta - (Bump | bumps). Matuta ya barabara.
3. Mzunguko wa barabarani - (Round about).
4. Rangi ya kaharabu - (amber).
5. Alama za barabarani huarifu, hutoa maelezo, huamuru, na pia hutoa tahadhari.
a) Taarifa (zinazoarifu)
b) Amri (zinazotoa amri)
c) Maelezo (zinazotoa maelezo)
d) Tahadhari (zinazotoa tahadhari)