Hotuba by
Olpha Janduko
6
Hotuba ni nini?
Soma hotuba ifuatayo.
"Mwalimu mkuu,naibu wa mwalimu mkuu,naibu wa raisi,baraza la mawaziri na wabunge hamjambo? Nimefurahi kuwaona nyote mmehudhuria mkutano huu ili tuzungumzie maswala yanayoikumba shule hii ya Amani.
Kwanza ni utovu wa nidhamu dhidi ya wanagenzi ambayo imesorota.Wanafunzi hawawatii walimu,viongozi wa shule na hata wazazi wao.Mnakumbuka juzi mzazi alileta malalamishi kuwa mwanawe hamsaidii na kazi ya nyumbani.Hata huyo mtoto amefika kiwango cha kumtusi mzazi.Kwa hivyo tushirikiane kuwarudi hao wanafunzi.
Pili,wanafunzi wengi huchelewa kufika shuleni.Kuwafanya kukosa masomo ya asubuhi.Na wengine pia hawafanyi kazi ya ziada ninatarajia viongozi wa wanafunzi tushirikiane kumaliza shida hiyo.
Nimegundua kuwa wanafunzi wengi wamerarua vile vitabu vya kusoma walivyopewa muhula uliopita.Waziri wa elimu pamoja na wabunge hakikisha mmeweka kanuni juu ya utunzi wa vitabu.
Nikimalizia,waziri wa afya,mifeji ya maji imeharibiwa na bunge la chekechea.Pia sisi sote tuzingatie usafi bungeni, jikoni, majilisi na vyooni.
6
Asante kwa kunisikiliza na ninatumaini kwamba sote tutashirikiana ili tuifanye shule yetu ifaulu na kupendeza. Mbarikiwe na Mola".
Maswali
- Ni nani anayetoa hotuba?
- Ni akina nani waliohudhuria kikao?
- Ni maswala yapi yametajwa?
- Ni bunge gani limeharibu mifereji?
- Usafi utazingatiwa sehemu gani?
Majibu
- Ni raisi wa shule.
- Mwalimu mkuu,naibu wake,naibu wa raisi,baraza la mawaziri na wabunge.
- Nidhamu,kuchelewa naa kutofanya kazi ya ziada,vitabu,mifereji na usafi.
- Ni bunge la chekechea.
- Sehemu ya bungeni,jikoni,majilisini na vyooni.