Mazungumzo by
Margaret Nguli
6
Tazama picha ifuatayo Kwa makini
Je unatambua hapa ni wapi? Hapa ni hospitalini.
Daktari anamtazama mgonjwa
MAZUNGUMZO
mazungumzo baina ya daktari na mgonjwa
(wagonjwa wameketi pambajioni wakinjojea kuitwa na daktari)
Daktari :mwingine tafadhari (mgonjwa anajitoma ndani na anonekana myonge sana).
Daktari :habari yako kijana?
Kijana :Mbaya kabisa daktari. (anaonekana akilengwa lengwa na machozi).
Daktari :Keti kijana (anaketi ) naitwa daktari Nguli nikusaidie vipi?
kijana :Daktari huwezi kunisaidia. Ninakufa, nina ugonjwa wa ukimwi. Niliambiwa na rafiki yangu kuna dawa za kunisaidia niishi siku chache zijazo. Naomba hizo dawa niweze kujipanga kabla sijafa.
Daktari :kijana sikiza kila mtu si daktari, je huyo rafikiyo amekupima. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza ukweli utakuweka huru. Chukua karatasi hii uipeleke kwenye maabara kisha urudishe matokeo hapa hapa.
Kijana :Ukweli upi daktari unaotafuta mimi huoni jinsi ambavyo nimedhoofika. Hebu nitazame mimi nimebaki mfupa tu. Ninaogopa kupimwa sina uhakika niko tayari.
Daktari :Sawa usiwe na wasiwasi lakini kabla ya hayo utashauliwa vilivyo na mhudumu wa afya katika chumba cha ushauri.
Kijana ; Sawa daktari lakini muda tunaopoteza tukiongea naona siku zangu zaendelea kupungua.
Daktari : Sawa, nenda mahali nimekutuma.
Kijana : Sawa daktari (kijana anatoka ina kuelekea kwenye chumba uchunguzi) huko anakuwa na mazungumzo na mshauri.
Kijana :(anarudi kwa daktari na karatasi mkononi) Haya daktari matokeo ndio hapa daktari.
Daktari :Keti (daktari anasoma matokeo kisha anatikisha kichwa).
Kijana :Sema daktari siku ngapi zimebaki? (kijana naonekana kujawa na hamaki)
Daktari :Matokeo si ya kufurahisha kijana lakini nataka uelewe fika kuwa lazima uwe na subira, daktari anaelezea kijana kuhusu ugonjwa wa ukimwi na jinsi ya kujikinga .
Kijana :Asante daktari hata hivyo nitajaribu niwezavyo kuelimisha wenzangu juu ya ugonjwa huu hatari.
Daktari :lakini kijana matokeo yako si ya ugonjwa huu wa ukimwi (kijana anasimama na kuruka ruka huku akimkubatia daktari)
Kijana :Mbona sikuelewi daktari?
Daktari :Wewe una ugonjwa wa kifua kikuu kijana kwa hivyo nitakupatia dawa na utadungwa sindano thelathini kwa siku thelathini mfululizo baada ya hapo afya yako itaimalika.
Kijana :Asante sana daktari. Nitafanya kila niwezavyo kuwashauri wenzangu wafanye juu chinI kufanyiwa uchunguzi. kuna watu wengi ambao wako kama mimi.
Daktari :Hii ni amali yangu.ukitaka kuwa na afya njema sharti utibiwe
Kijana :Asante sana daktari kwaheri(kijana anatoka huku akitabasamu)