Kivumishi ‘OTE’ by
Joyce Muigai
6
Ote ni kivumishi cha kutaja jumla au pamoja au kitu kizima bila kugawanya au kutengganisha.
Mfano
Mlo wote au jumba lote Ina maana kuwa pamoja au jumla au mzima bila kuacha kingine kando.
Mifano katika sentensi
•Nguo yote ilichafuliwa.
•Chakula chote kililiwa.
•Jumba lote lilisafiswa.
•O--ote hutumika kuonyesha kati ya vingine au miongoni mwa. Vitu kadhaa wala si vyote.
•Baadhi tu, bila kuchagua wala kubagua.
mifano katika sentensi
•Mwanafunzi yeyote anaitwa na mwalimu.
•Chochote kiingiacho mjini si haramu.
•Vivumishi ote na o--ote huchukua kiambishijina hivyo huchukuana na ngeli husika kwa mwingiliano thabiti.
ZOEZI
•1 Fujo ---- za kisiasa hazifai kamwe na zinafaa kuzikwa katika kaburi la sahau.
•2 Ukimwi ni uwele mbaya kwa mja---------
•3 Watu wakiishi bila mpaka -------- wa maisha, watakuwa pakashume
•4 Ajira-------- kwa watoto hafai.
•5 Mitume --------watakuwa na mkutano wao kesho.
MAJIBU
- Zozote
- Yeyote
- Wowote
- oyote
- Wowote
6
-ote hutumiwa kumaanisha kila kitu,bila kubakiza au kitu kizima
Ngeli ya a_wa
Ndege wote ameliwa.
Ndege wote wameliwa.
Ngeli ya ki _vi
Chakula chote kimeliwa.
Vyakula vyote vimeliwa.
Ngeli ya li _ya
Chungwa lote limeiva
Machungwa yote yameiva.
Ngeli ya u_i
Mkate wote umeliwa.
Mikate yote imeliwa.
Ngeli ya i_zi
Nguo yote imeraruka.
Nguo zote zimeraruka.
Ngeli ya ku_ku
Kulia kote kuna chukiza.
Kulia kote kunachukiza.
Ngeli ya pa_ku_mu
Shuleni pote pana.
Shuleni kote kuna maua.
Shuleni mote mna maua.
Zoezi
Kamilisha sentensi zifuatazo kwakutumia _ ote.
1.Kalamu _____ zinaandika vizuri.
2.Mahali _____ pamejaa maji.
3.Dawati _____ limepakwa rangi.
4.Kiti _____ ni cheusi..
5.Ng’ombe _____ wamepelekwamalishoni.
Majibu
1.Zote
2.pote
3.lote
4.chote
5.wote