6
Ote ni kivumishi cha kutaja jumla au pamoja au kitu kizima bila kugawanya au kutengganisha.
Mlo wote au jumba lote. Ina maana kuwa pamoja au jumla au mzima bila kuacha kingine kando.
O--ote hutumika kuonyesha kati ya vingine au miongoni mwa. Vitu kadhaa wala si vyote. Baadhi tu, bila kuchagua wala kubagua.
Vivumishi ote na o--ote huchukua kiambishijina hivyo huchukuana na ngeli husika kwa mwingiliano thabiti.
Nominoambata huuundwa kwa nomino mbili (majina mawili) ambazo huambatanishwa na kuwa neno mja.aghalabu maneno yanayounganishwa hayana uhusiano wowote kimaana.
Askari + kanzu =askarikanzu
mwana+ mkiwa= mwanamkiwa
Mwana+nchi= mwananchi
Mbwa + mwitu=mbwamwitu
Pembe+tatu=pembetatu
kiinua+mgongo=kiinuamgongo
nusu +kipenyo= nusukipenyo
Simba +marara=simbamarara
KUMBUKA ;maana ya neno yaweza kubadilika kabisa nomino mbili zinapoambanishwa.
simbamarara (a-wa)---fisi mkubwa
Kivunjajungu (a--wa)---mdudu jamii ya panzi
Mjamziti (a-wa)---mwanamke aliyehimili
Mtambaapanya(u -I) mboriti(miti) inayoshikilia paa
Kiamshakinywa (ki-vi)--chakula cha kwanza cha
asubuhi.
Mwanambuzi (a-wa)--mtoto wa mbuzi.
Tumia neno mwana kuunda nomno ambata kumi.
Mfano
Mwana+ sheria=mwanasheria
mwana+mke+mwanamke.