Kirejeshi "NDI" by
Ruth Odachi
6
Kirejeshi -ndi hutumika katika kukubali kwa kusisitiza nomino, jambo, au wazo ili kuthibitisha ukweli.
Aidha
Kirejeshi -ndi pia hufanana na kirejeshi amba kwa vile huchukua viambishi ngeli kulingana na upatanisho wa kisarufi.
Je,unafikiria huyu ni nani ?
Je, unafikiria huyu ni nani?
Huyu ndiye mtalii uliyemwona.
Hawa ni watalii
Hawa ndio watalii ambao huzuru Kenya.
Hili ni
Tumia -ndi
Jani hilo ndilo lililonipendeza.
Rinda hili ndilo lake.
Nyumba hii ndiyo nzuri
ZOEZI
- Tunga sentensi ukitumia maneno yafuatayo pamoja na kirejeshi -ndi umoja na wingi:
- Tunga sentensi ukitumia maneno haya.
1) Chumba.
2)Nguo.
3) Maji
Zoezi la ziada
Kamilisha sentensi ukitumia kirejeshi -ndi kwa ufasaha.
1) Shati---------kubwa kuliko kaptura.
2) Sukari---------inayopatikana dukani.
3) Uzi huu-------ulipotea.
4) Vyumba vile------- vitauzwa.
5) Meza zenu-------mpya.
Majibu ya zoezi la ziada
1) Shati ndilo kubwa kuliko kaptura.
2)Sukari ndiyo inayopatikana dukani.
3) Uzi huu ndio uliopotea.
4) Vyumba vile ndivyo vitauzwa.
5) Meza zenu ndizo mpya.