Matumizi ya ‘enye’ na ‘enyewe’ kulingana na ngeli by
Margaret Nguli
6
Matumizi ya enye na enyewe
- Enye hutumika kuonyesha hali ya kumiliki au kuwa na kitu fulani kinachotajwa unapotumia
- ENYE katika sentensi ,usifuatanishe ---enye na kitenzi.katika sarufi, sentensi yako haitakuwa sanifu.
MIFANO KATIKA SENTENSI
Mwalimu mwenye gari = gari ni lake
mtoto mwenye mzigo = ana mzigo au mzigo ni wake
USISEME
•gari lenye linabeba
•Mtu mwenye anakimbia
•Mtoto mwenye anakuja
SEMA
•Mtoto ambaye anakuja/mtoto anayekuja/mtoto ajaye
•Mtu ambaye anakmbia/mtu anayekimbia/mtu akimbiaye.
•gari ambalo linabeba /gari linalobeba/gari libebalo.
ENYEWE
NI kivumishi cha pekee ambacho huunganishwa na kiambishi awali ili kuafiki sarufi.kivumishi hiki huleta dhana tofauti katika matamshi ya lugha.
MIFANO
Hutumi kuonyesha mmiliki wa kitu
•Sentensi
•Kitabu hiki ni cha mwenyewe(pasi na kumtaja jina)
•Mtoto mwenyewe ameanguka akaumia(pasi na kumtaja jina)
•Gari lile limeegeshwa hapa na mwenyewe(pasi na kumtaja jina)
Hutumika kuonyesha kuwa kitu kilichokusudiwa bila kubadilishwa nakingine
•1 mtoto mwenyewe amefika mapema kabla yangu.
•2 kitabu kilichochapishwa ni chenyewe.
•3 uwanja wenyewe umetunzwa ukatunzika
Hutumi kuonyesha kuwa nomino iliyotajwa iljisababisha pasina msababishi. hutumika badala ya kiambishi. Ji-- cha nafsi.
•1 mtoto alianguka mwenyewe.
•2 Gari lile liianguka lenyewe.
•3 Mti mkubwa ulianguka wenyewe.
Hutumi kama kiwakilishi.
•1 Mwenyewe amechukua kitabu kilichokuwa hapo
•2 wenyewe tunafaa kutekeleza wajibu wetu ili amani idumu.
•3 chenyewe kilianguka chini kikavunjika.
TANBIHI
VIVUMISHI HALISI
•ENYE NA ENYEWE.
•lazima vichukue viambishi vya ngeli
ZOEZI
- JIKO------lina makaa
- Sahani-----uchafu haitumiki.
- mtoto------ni----sauti nzuri.
- Barabara-----utelezi haipitiki.
- kitabu cha-------hakisomwi bila idhini yake.
- mwalimu----- uadilifu gangeni hukuza jina lake-----.