Tarakimu by
Olpha Janduko
6
Tarakimu kuanzia 100,000-1,000,000.
Andika tarakimu hizi kwa maneno.
Watu 107,333
Miti 808,696
Viti 732,589
Magari 1,484,203
Kalamu 1,012,969
Majibu
- 107,333 - Watu mia moja na saba elfu,mia tatu thelathini na watatu.
- 808,696 - Miti mia nane na nane elfu,mia sita tisini na sita.
- 732,589 - Viti Mia saba thelathini na mbili elfu,mia tano themanini na tisa.
- 1,484,203 - Magari milioni moja,mia nne themanini na nne elfu,mia mbili na matatu.
- 1,012,969 - Kalamu milioni moja,kumi na mbili elfu,mia tisa sitini na tisa.
Zoezi
Tunga sentensi ukitumia tarakimu zifuatazo.
Majibu
- 508,659 - Wanafunzi mia tano na nane elfu,mia sita hamsini na tisa
- 400,069 - Sahani mia nne elfu na sitini na tisa.
- 783,421-Miche mia saba themanini na tatu elfu,mia nne ishirini na moja.
- 1,020,003 - Mayai milioni moja,ishirini elfu,na tatu.
- 1,008,106 - Vitabu milioni moja,nane elfu,mia moja na sita.