Nomino ambata by
Margaret Nguli
6
Nomino ambata huuundwa kwa nomino mbili (majina mawili) ambazo huambatanishwa na kuwa neno mja. Aghalabu maneno yanayounganishwa hayana uhusiano wowote kimaana.
Mifano
- Askari + kanzu = askarikanzu
- mwana + mkiwa = mwanamkiwa
- Mwana +nchi = mwananchi
- Mbwa + mwitu = mbwamwitu
- Pembe + tatu = pembetatu
- Kiinua + mgongo = kiinuamgongo
- Nusu + kipenyo = nusukipenyo
- Simba + marara = simbamarara
KUMBUKA ;maana ya neno yaweza kubadilika kabisa nomino mbili zinapoambanishwa.
MIFANO ZAIDI NA MAELEZO YAKE.
- Simbamarara (a-wa) ____ fisi mkubwa.
- Kivunjajungu (a-wa) ____ mdudu jamii ya panzi.
- Mjamziti (a-wa) ____ mwanamke aliyehimili.
- Mtambaapanya(u -I) ____ mboriti (miti) inayoshikilia paa.
- Kiamshakinywa (ki-vi) ____ chakula cha kwanza cha asubuhi.
- Mwanambuzi (a-wa) ____ mtoto wa mbuzi.
ZOEZI
Tumia neno mwana kuunda nomIno ambata kumi.
Mfano
- Mwana+ sheria = mwanasheria
- mwana + mke = mwanamke
Tazama mifano zaidi
- Mwana jeshi
- Mwanasheria
- Mwanaserere
- Mwanamaji
- Mwanandondi
- Mwanadamu
- Mwanambuzi
- Mwanamkiwa
- Mwanahewa