Insha ya hadithi

- Katika insha ya hadithi, mtahiniwa anatakikana kutunga hadithi yake mwenyewe na kuiandika Je, ni yapi anayostahili kuyaelewa?

  • Usemi wa kutumia kulingana na swali: Mtahiniwa anaweza kutumia usemi wa kauli halisi au usemi wa taarifa. Yaangalie maswali haya mawili.
  • “Paukwa?” Babu alianza. Nasi tulimjibu “pakawa,” “ Hapo zamani …”. Aliendelea.
  • … Tulimshukuru nyanya kwa kutusimulia hadithi iliyokuwa na mafunzo tele. Utaona ya kwamba, katika swali la kwanza, ni lazima mtahiniwa atumie usemi wa kauli halisi. Katika swali la pili, mtahiniwa anaweza kutumia usemi wa kauli halisi au usemi wa taarifa. Hata hivyo,ni bora kutumia usemi wa kauli halisi. Katika insha ya hadithi.

 

Unapoandika insha ya hadithi:

  1. Lazima insha yako iwe na kichwa.
  2. Tunga au buni hadithi yako. Kamwe usi•nakili hadithi uliyoisoma vitabuni kwani utapoteza alama au maksi za ubunifu. (kumbuka 14)
  3. Hakikisha wahusika wako au mhusika wako ni binadamu wala si mnyama.
  4. Katika aya ya mwisho, toa funzo la hadithi uliyoandika.

Zoezi

Fuata maagizo uliyopewa uandike insha ya hadithi.

Andika insha ukianza:

  • "Paukwa," nyanya alianza.
  • Tulipokusanyika pale sebuleni, nyanya aliianza hadithi yake.
  • Andika insha ya hadithi na uitamatishe hivi: … Tulimshukuru babu kwa kututolea hadithi yenye mafunzo tele.
  • Andika insha ya hadithi na uitamatishe hivi: … Kwa kweli hadithi hiyo ilitupendeza sana.