Kituo kikuu
Kituo kikuu/nukta/kikomo/kitone ( . )
Hutumika:
- Mwishoni mwa sentensi: k.m tutafika alfajiri na mapema.
- Kufupisha maneno: S.L.P. (Sanduku la posta).
Bw. Juma (Bwana Juma)
- Kutenga kiwango cha kitu kama vile fedha, kilomita, kilo n.k. Sh 6.80 (shilingi sita na senti themanini).
- Kilomita 2.5 (kilomita mbili na nusu).