Kistari kifupi 
							
								
							
								Kistari kifupi ( - ) 
Hutumika:
- Kuonyesha mzizi wa neno k.m. -zuri, -baya, -erevu.
- Kuendeleza neno linapokatwa katika sentensi mwishoni mwa mstari k.m Kitabu chenyewe kili- gharimu pesa nyingi. Somo la Jiografia lina- pendeza wanafunzi wengi.
-  Kusisitiza sauti k.m Walimcheka ha-ha-ha kwa ujuha wake.

- Kuunganisha tarakimu kuonyesha mwanzo hadi mwisho k.m Alikuwa mkurugenzi mkuu 1991 - 2006. v) Alifunza Kiswahili Januari - Oktoba. Katika uandishi wa tarehe k.m. 7 - 4 - 2006.