Nukta za dukuduku 
							
								
							
								Nukta za dukuduku ( … ) 
Hutumika:
- Kuonyeshea kuendelea kwa maelezo fulani k.m. Tukikutana sitamzungumzia kwa kuwa … 
- Kuonyeshea maelezo yaliyo wazi kwa msikilizaji k.m. Niliamua kurejea kwetu mambo yaliponiendea mrama. Kama mjuavyo, ng’ombe akivunjika guu malishoni … 
- Kuonyeshea kuwa kuna maelezo mengine yaliyotangulia lakini hayajaandikwa k.m. … na ni kweli lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani likija.