Ngeli
a) Kupanga nomino kwa kuzingatia uwiano wa silabi za kwanza za nomino hizo. Yaani, nomino ambazo zina silabi sawa za mwanzo huwekwa katika kikundi kimoja.Huu ni mtindo wa viambishijina k w a kuwa tunafuata viambishi vya nomino/jina/nauni.
b) Kupanga nomino kwa kuzingatia uwiano wa silabi za kwanza za kiarifa. Nomino zote ambazo zikitumiwa katika sentensi, viarifu vinavyozirejelea huwa na viambishi sawa huwekwa katika kikundi kimoja. Huu ni mtindo wa viambishirifa au viambishi ngeli/viambishi vitenzi.
1. A- WA
2. KI-VI
3. LI-YA
4. I-I
5. I-ZI
6. U-I
7. U-ZI
8. U-U
9. U-YA
10. YA-YA
11. MAHALI:
12. PA-PA
13. KU-KU
14. MU-MU
Ili kuepuka hali ya ukanganyi, kitabu hiki kimetumia utaratibu wa viambishirifa au viambishingeli.
U-ZI
Ukuta unapakwa rangi. Kuta zinapakwa rangi.
Ulimi unaongea. Ndimi zinaongea.
U-I
Mlango umefungwa. Milango imefungwa.
Mlima unateleza. Milima inateleza.
U-U
Uji umeiva. Uji umeiva.
Usafi unaridhisha. Usafi unaridhisha.
U-YA
Upishi wake umekawia. Mapishi yao yamekawia.
Uwele umeanikwa. Mawele yameanikwa.
I-I
Chai imepikwa. Chai imepikwa.
Baridi inaniathiri. Baridi inatuathiri.
YA-YA
Marashi yananukia. Marashi yananukia.
Maji yametiwa dawa. Maji yametiwa dawa.
PA-PA Sokoni pana wateja wengi. Sokoni pana wateja wengi.
Darasani pana mwanafunzi. Darasani pana mwanafunzi.
M-M
Sokoni muna wateja wengi. Sokoni muna wateja wengi.
Darasani muna wanafunzi. Darasani muna wanafunzi.
KU-KU
Sokoni kuna wateja wengi. Sokoni kuna wateja wengi.
Darasani kuna wanafunzi. Darasani kuna wanafunzi.
Kucheka kwake kunapendeza. Kucheka kwao kunapendeza.
Kulima kule ni kuzuri. Kulima kule ni kuzuri.
Muhimu:
1. Jua nomino ambazo hupatikana katika ngeli yoyote ile.
2: Elewa vivumishi vya ngeli hiyo.
Kivumishi -enyewe
Umoja: Tawi limevunjika lenyewe.
Wingi: Matawi yamevunjika yenyewe.
Kivumishi -ote
Hutumika kuonyeshea ukamilifu wa kila sehemu k.m
Darasa lote limefurika.
Umoja: Darasa lote limepambika.
Wingi: Madarasa yote yamepambika.
Kivumishi -o-ote
Umoja: Mpishi atalitumia jiko l o l o t e litakalopatikana.
Wingi: Wapishi watayatumia majiko yoyote yatakayopatikana.
Kivumishi -ngi
Umoja: Uwanjani hakuna vumbi jingi.
Wingi: Uwanjani hakuna mavumbi mengi.
Muhimu
Kivumishi jingi hutumika kwa nomino chache tu katika ngeli hii ya LI-YA. k.m vumbi, tunda, gari n.k.
Kivumishi -ngine
Umoja: Nitalijibu swali jingine iwapo nitaulizwa.
Wingi: Tutayajibu maswali mengine iwapo tutaulizwa.
Kiulizi -pi?
Umoja: Baba alilitumia gari lipi?
Wingi: Akina baba waliyatumia magari yapi?