- Ngeli ya KU huonyesha mahali HUKU, HUKO, KULE, ambako ni mahali kusiko dhahiri au wazi; si maalum hata kama ni karibu nasi.
- Ngeli hii hujumuisha aina mbili za maneno.
• Nomino za mahali.
• Vitenzi vinavyoanza kwa silabi ku.
N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HUKU, HUKO, KULE.
Mifano:
a) Nyumbani huku kunapendeza.
b) Nyumbani huko kunapendeza.
c) Nyumbani kule hakupendezi.
1. Kiwakilishi amba-
Kucheka ambako anacheka kunapendeza.
Machimboni ambako kunachimbwa hakuna mawe imara.
2. “O” rejeshi
Kucheka anakocheka kunapendeza.
Machimboni kunakochimbwa kuna mawe imara.
3. Ndi- ya kusisitiza
Kuogelea ndiko kulikonichelewesha.
Nyumbani kwa Musa ndiko kule.
4. Si- ya kukataa
Kuogelea siko kulikonichelewesha.+
Nyumbani kwa Musa siko kule.
5. Na- ya kirejelei
Kibandani huku nako kuna vimelea wengi.
Kusoma nako kuna faida.
6. Viashiria/vionyeshi: a) huku, b) huko, c) kule.
- Viashiria/vionyeshi visisitizi: kuku huku, kuko huko, kule kule.
- Viashiria/vionyeshi radidi: huku huku, huko huko, kile kile.
7. Kivumishi -enye
Kushirikiana kwenye manufaa kunapendeza.
Mtoni kwenye samaki huvutia wavuvi.
8. Kivumishi -enyewe.
Kuogelea kwenyewe kulichosha.
Mtoni kwenyewe hakuna samaki wengi.
9. Kivumishi -ote
Mezani kote kuna vitabu.
Kujibidiisha kwao kote hakukuwawezesha washinde.
10. Kivumishi -o-ote
Nitakaa kokote nitakakoonyeshwa.
Hatutashiriki kucheza kokote kule.
11. Kivumishi -ngi
Kulalamika kwingi hakufai.
Hotelini kwingi kumejaa watalii.
12. Kivumishi -ngine
Kuvaa kwingine kunaaibisha.
Viwanjani kwingine hakukuwa na michezo.
13. Kiulizi -pi?
Ni kusoma kupi kulikotuzwa?
Kwa vyovyote vile usichanganye vivumishi vya ngeli hizo tatu za mahali. Kwa kawaida vivumishi vya: