A -unganifu hutumika kuonyeshea uhusiano kati ya nomino mbili au vitenzi.
A-unganifu hubadilika kutoka ngeli moja hadi nyingine.
Tazama jedwali lifwatalo
| Ngeli | Nomino | Kiashiria(i) | Kiwakilishi | Matumizi | 
 | 
| KI - VI | Kioo | Hiki | Ki | Nitakiosha kioo | |
| Vioo | Hivi | Vi | Tutaviosha vioo | ||
| LI - YA | Tawi | Hili | Li | Unalikata tawi | |
| Matawi | Haya | Ya | Mnayakata matawi | ||
| U - I | Msumeno | Huu | U | Anaununua msumeno | |
| Misumeno | Hii | I | Wanainunua misumeno | ||
| U - U | Ugomvi | Huu | U | Anausuluhisha ugomvi | |
| 
 | |||||
| I - ZI | Nguo | Hii | I | Nitaifua nguo | |
| nguo | hizi | zi | Tutazifua nguo | ||
| U - YA | Uwele | huu | u | Anaudondoa uwele | |
| mawele | haya | ya | Anayadondoa mawele | ||
| YA - YA | Manukato | haya | ya | Anayanunua manukato | |
| 
 | 
 | 
 | 
 | ||
| U - ZI | Ufa | Huu | U | Anauziba ufa | |
| Nyufa | hizi | zi | Wanaziziba nyufa | ||
| I - I | Hewa | hii | i | Naipumua hewa | |
| PA - PA | Sokoni | hapa | pa | Aanapapendelea sokoni | |
| KUKU | kucheza | huku | ku | Ninakupendelea kucheza | |
| M - M | sakafuni | humu | m | Anamwosha sakafuni |  | 
Chagua jibu sahihi
1.Kibago _____ ( ya, cha, la, wa) jikoni kimevunjika.
2. Nywele _____ ( wa, ya, za, vya) watoto hunyolewa.
3. Unga _____ ( ya, wa, cha, za) ugali ni mweupe sana.
4. Maskanini _____ ( kwa, pa, mwa, ya) mchwa ni kichuguuni.
5. Rafiki _____ ( ya, wa, la, cha) kweli ni akufaaye kwa dhiki.
6. Chumbani _____ ( cha, ya, la, pa) mama husafishwa kila siku.
7. Mitume _____ ( ya,wa, za,mwa) Mungu ni watakatifu.
8. Chupa ____ ( wa,cha,ya,la) dawa huwekwa mbali.
9. Shati _____ ( ya, la,cha, za) mtoto ni safi.
10. Waridi _____ ( la, wa, ya, za) arusi hunukia.