Kwa lugha rahisi na ya moja kwa moja tunaweza kusema nafsi ni sawa na “mtu”. Katika lugha ya Kiswahili tunazo nafsi tatu:
Nafsi ya kwanza Mimi – huwakilishwa na ni.

Sisi – huwakilishwa na tu.

Nafsi ya pili Wewe – huwakilishwa na u.

Nyinyi – huwakilishwa na m.

Nafsi ya tatu Yeye – huwakilishwa na a.

Wao – huwakilishwa na wa.

Viwakilishi
Kiwakilishi ni neno au silabi inayosimama badala ya nomino au kitenzi. Viwakilishi vya nafsi ni kama vifuatavyo.
Nafsi Kiwakilishi Matumizi
| Nafsi ya kwanza | Mimi | Nitasoma kwa bidii | 
| Sisi | Tutasoma kwa bidii | |
| Nafsi ya pili | Wewe | Utasoma kwa bidii | 
| Nyinyi | Mtasoma kwa bidii | |
| Nafsi ya tatu | Yeye | Atasoma kwa bidii | 
| Wao | Watasoma kwa bidii 
 | 
Iwapo kitenzi kitanyambuliwa kiwe katika hali ya kufanyia, kiwakilishi cha wewe hubadilika kutoka u na kuwa ku. k.m
Utaandika barua (kufanya) - Nitakuandikia barua (kufanyia).
Yeye nacho huwa m badala ya a k.m. Alimcheka (kufanya) - Nilimcheka (kufanyia)
Viashiria vinaweza kutumika kama viwakilishi. Kiashiria huwa kiwakilishi kinapotumika badala ya nomino au kitenzi kinachoashiriwa. Kwa hivyo, hakitaandamana na nomino au kitenzi husika.
Ziangalie sentensi zifuatazo: Mtu huyu ana bidii - kiashiria Mtu huyu ana bidii, yule ni mzembe. Huyu – kiashiria Yule – kiwakilishi – kinawakilisha mtu wa pili (ambaye ni mzembe).