- Kinyume ni sawa na “upande ule mwingine”.
- Kunavyo vinyume vya vitenzi na vya nomino.
Mifano:-
Cheka (kitenzi); lia (kitenzi kinyume cha cheka);
Utajiri (nomino) – umaskini (nomino).
Baadhi ya vitenzi hunyambuliwa ili kupata kinyume chao k.m
vaa – vua,
Ziba - zibua,
Tia - toa,
Muhimu
- Ni vyema uelewe mnyambuliko wa kitenzi kabla hujataja kinyume.
- Hii ni kwa sababu mnyambuliko wa vitenzi unaathiri hali ya kinyume k.m. tanda -tandua, tandika -tanduka, valia - vulia, valika - vulika
mwanamume – mwanamke,
mfarika – beberu,
kijakazi – kitwana n.k.
kasirika – furahi,
cheka – lia,
meza – tema,
uza – nunua,
giza – mwangaza,
usiku – mchana,
refu – fupi,
kimbia – tembea,
amka – lala,
tabasamu – nuna,