Ukanushaji 
							
								
							
								Ukanushaji 
Ukanushaji ni sawa na kukataa.
- Ukanushaji wa nyakati Ukanushaji wa kiarifu sawa hutofautiana kutokana na nyakati. Iangalie mifano ifuatayo.
Mtoto anacheka – Mtoto hacheki.

Mtoto amecheka – Mtoto hajacheka. Mtoto atacheka – Mtoto hatacheka. Mtoto alicheka– Mtoto hakucheka. Mtoto hucheka – Mtoto huwa hacheki.
- Ukanushaji wa kiunganishi “na“ Kiunganishi na hukanushwa kwa kiunganishi wala k.m. Alifika na akapumzika - Hakufika wala hakupumzika.
- Ukanushaji wa “ku-” ya kitenzi Vitenzi vilivyo na viambishi k u – hukanushwa kwa kuto -k.m. kusoma – kutosoma, kulia – kutolia, kula – kutokula.

- Ukanushaji wa “ki-” cha masharti Ki– cha masharti pia huitwa ki– cha lazima. Hii ni kwa sababu matokeo fulani lazima yetegemee tukio fulani k.m. Ukisoma kwa bidii utafua dafu (yaani lazima/sharti usome kwa bidii ili ufue dafu).
Ukanushaji  wake ni –sipo-  k.m  M kiniita
nitaitika - M sipo niita sitaitika;  Aki ja ataniona
– A sipokuja  hataniona.
Ukanushaji wa – nge– ya utegemeano 
Hukanushwa kwa kutumia – singe – k .m .Ningekuwa na uwezo  ni ngeenda ughaibuni
Nisingekuwa na uwezo nisingeenda ughaibuni.
 
Ukanushaji  wa – ngali–  ya u tegemeano
Hukanushwa kwa kutumia - singali - k.m
Tungalimakinika tungalifua dafu
Tusingali makinika  tu singali fua  dafu.
 
Ukanushaji wa “ndi-” ya kusisitiza
Hukanushwa  kwa  kutumia  -si- ya kukataa
k.m. Kitumbua hiki ndichonilichopika
Kitumbua hiki  sicho nilichopika.
Ukanushaji wa kiarifu chenye  ʻ o rejeshi  mwishoni
Kiarifu hicho hakikanushwi bali kiari
kinachokifuata ndicho  kinachokanushwa k.m
Mtoto achezaye  ninamjua–  Mtoto achezaye simjui.

Ukanushaji  wa k iunganishi  n i huwa  s i
k.m Mkoba huu  ni wangu
Mkoba huu  si  wangu

- Ukanushaji wake ni –sipo-k.m Mkiniita nitaitika - Msiponiita sitaitika; Akija ataniona –Asipokuja hataniona.
- Ukanushaji wa –nge– ya utegemeano Hukanushwa kwa kutumia – singe – k.m. Ningekuwa na uwezo ningeenda ughaibuni -Nisinge kuwa na uwezo nisingeenda ughaibuni.
- Ukanushaji wa –ngali– ya utegemeano Hukanushwa kwa kutumia - singali -k.m. Tungalimakinika tungalifua dafu – Tusingalimakinika tusingalifua dafu.
- Ukanushaji wa “ndi-” ya kusisitiza Hukanushwa kwa kutumia -si-ya kukataa k.m. Kitumbua hiki ndicho nilichopika -Kitumbua hiki sicho nilichopika.
- Ukanushaji wa kiarifu chenye •o• rejeshi mwishoni Kiarifu hicho hakikanushwi bali kiarifu kinachokifuata ndicho kinachokanushwa k.m Mtoto achezaye ninamjua – Mtoto achezaye simjui.
- Ukanushaji wa kiunganishi ni huwa si k.m Mkoba huu ni wangu Mkoba huu si wangu