Usemi wa kauli halisi
- Usemi wa kauli halisi pia huitwa usemi wa moja kwa moja.
- Katika usemi huu maneno ya msemaji hunukuliwa moja kwa moja jinsi alivyoyatamka. Kwa hivyo, sheria fulani huzingatiwa.
- Alama za kunukuu hutumika k.m. “Kitabu hiki ni changu,“ mwanafunzi alisema.
- Alama za kuulizia hutumika k.m. “Je, umemwona Hamisi?” dada aliuliza.
- Alama za hisi hutumika k.m. “Lo! Hamwogopi nyoka!” Mwalimu alishangaa.
- Wakati wowote hutumika k.m. “Nitaenda Mombasa,” shangazi alisema; “Walifika jana,” mwenyeji alieleza. Katika matumizi ya kauli halisi wanafunzi hukumbana na tatizo moja sugu: jinsi ya kutumia herufi kubwa, koma na kikomo.
Tazama sentensi zifuatazo:
- Mama alisema, “Leta kikombe.”
- “Leta kikombe,” mama alisema. Ukiziangalia sentensi hizi mbili, utaona kuwa, matumizi ya koma na kikomo ni tofauti.
Ukiziangalia sentensi hizi mbili, utaona kuwa, matumizi ya koma na kikomo ni tofauti.
- Iwapo sentensi inaanza na maelezo ya mnenaji, koma hufuata maelezo hayo nacho
kituo huwekwa mwishoni mwa maneno
yanayonukuliwa k.m. Mwalimu aliniambia,
“Kiweke kitabu chako mezani.”
- Iwapo sentensi inaanza na maneno yanayonukuliwa, koma huwekwa
mwishoni mwa maneno hayo nacho kituo.
huwekwa mwishoni mwa maelezo ya mnenaji k.m. “Kiweke kitabu chako
mezani,” mwalimu aliniambia.
- Maelezo yanayofuata maneno yanayonukuliwa huanza kwa herufi ndogo k.m. “Mkate huu ni mtamu,” mtoto alisema.
- Unapomnukuu mzungu mzaji, alama za kunukuu huwekwa baada ya kuweka koma,kituo, kihisi, kiulizi:
Sahihi makosa
- Iwapo sentensi inaanza na maelezo ya mnenaji, koma hufuata maelezo hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maneno yanayonukuliwa k.m. Mwalimu aliniambia, “Kiweke kitabu chako mezani.”
- Iwapo sentensi inaanza na maneno yanayonukuliwa, koma huwekwa mwishoni mwa maneno hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maelezo ya mnenaji k.m. “Kiweke kitabu chako mezani,” mwalimu aliniambia.
- Maelezo yanayofuata maneno yanayonukuliwa huanza kwa herufi ndogo k.m.
“Mkate huu ni mtamu,” mtoto alisema.
Unapomnukuu mzungumzaji, alama za kunukuu huwekwa baada ya kuweka koma, kituo, kihisi, kiulizi: Sahihi makosa “--------------,” “--------------”,