Matumizi ya 'huku' 
							
								
							
								Huku hutumika kwa njia tatu:
- Huku ya mahali; Huku shuleni kunapendeza. Huku tunakosomea ni kutulivu.

-  Huku ya wakati Huonyeshea kuwa vitendo viwili vinafanyika wakati mmoja: k.m. Nyanya alituhadithia huku akipika ugali; Huku akiongea, mwalimu aliandika ubaoni.
-  Huku ya kiashiria Hutumika katika ngeli ya KU-KU kuashiria, vitenzi Kucheza huku kunapendeza. Kusoma huku kunafaidi.
