- Ngeli ya MU huonyesha HUMU, HUMO, MLE, ambamo ni ndani. Kwa mfano: Chumbani, shimoni, nyumbani, ama mafichoni.
- Viarifu vya ngeli hii huanza kwa silabi mu ndiposa inaitwa ngeli ya mahali ya mu-mu k.m. Sokoni mmejaa wauzaji.
N/B Jina lolote linaweza kupachikwa kiambishi tamati -ni, nalo likawa au likageuka kuwa mahali HUMU, HUMO, MLE.
Mifano:
a) Maskanini humu mna Bi. Harusi.
b) Maskanini humo mna Bi. Harusi.
c) Maskanini mle mna Bi. Harusi.
1. 'O' rejeshi
Sakafuni anamofagia munateleza.
2. Ndi- ya kusisitiza
Hamamuni alimoogea ndimo humu.
3. Si- ya kukataa
Hamamuni alimoogea simo humu.
4. Na- ya kirejelei
Humu namo muna watoto wengi.
5. Viashiria/vionyeshi
humu humo mle
mumu humu, mumo humo, mle mle.
humu humu, humo humo, mle mle.
6. Kivumishi -enye.
Sokoni mwenye wateja muna kelele.
7. Kivumishi -enyewe.
Tuliogelea mtoni mwenyewe.
8. Kivumishi -ote.
Mezani mote muna vitabu.
9. Kivumishi -o-ote.
Nitakaa momote nitakamoonyeshwa.
10. Kivumishi -ngi.
Hotelini mwingi muna starehe.
11. Kivumishi -ngine.
Amehamia mjini mwingine.
12. Kiulizi –pi?
Mjomba alienda shuleni mupi?