Heshima na adabu
Lugha ya heshima na adabu
- Lugha ya heshima hutumika kutajia mtu na hata mahali mbalimbali.
- Ni vizuri unapoongea na watu utumie maneno ya heshima la sivyo hata nawe hutaheshimiwa.
- Siti: Jina la heshima la mwanamke. Hutumika kabla ya jina lake.
- Bwana: Jina la heshima kwa mwanamume.
- Bibi: Jina la heshima kwa mwanamke.
- Nana: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamke.
- Mwinyi: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamume.
- Muadhama: Neno la heshima la kumwitia mtu maarufu (mheshimiwa)
- Kibibi: Tamko la kumwita mtoto mwanamke.
- Hayati: Marehemu:
Majina ya heshima ya kumtajia mtu
Mwendazake: aliyeaga dunia
Maneno ya heshima ya kuitikia
Abe hutumika na wanawake kuitikia wanapoitwa.
Bee, Beka, Naam: Neno la kuitikia kwa heshima.
Maneno ya adabu na unyenyekevu
- Tafadhali: Neno la heshima la kumwomba mtu afanye jambo kwa niaba yako.
- Shikamoo: Salamu ya heshima itolewayo kwa mtu aliyekuzidi umri.
- Samahani: Neno la kuombea msamaha. Neno la kuomba upewe nafasi au usikilizwe.
- Asante: Neno la kuonyesha shukrani kwa yale uliyotendewa.
- Ninasikitika:Neno la kuonyeshea hisia za huruma au kuionea hali ya mtu huruma.
- Simile: Neno la adabu la kuomba kupishwa njia.
- Ashakum: Neno la kuombea msamha kabla ya kusema jambo unalofikiria linaweza kumwudhi mtu anayekusikiliza.
- Mjamzito: Mwanamke aliyebeba mimba.
- Kujifungua:Kupata mtoto.
- Msalani/pembeni:Pahali pa kwendea haja.
- Pole: Neno la kumwonea mtu huruma au kumsikitikia kutokana na hali mbaya k.v. ugonjwa, kuumia n.k.