Methali |
---|
Maamkizi |
Heshima na adabu |
Vitate |
Semi na nahau |
Tashbihi |
Istiara |
Shada/takriri |
Tanakali |
Ushairi |
Vitendawili |
Tashbihi jozi |
Maswali kadirifu |
Vitate ni maneno ambayo matamshi yake yanakaribiana lakini maana ni tofauti.
Mifano ya vitate
vua – toa nguo
fua – osha nguo
wasaa – muda
fursa wasa – toa nasaha
pishi – chombo cha kupimia nafaka
bishi – enye kupenda ugomvi
kata – lokesheni
kataa – kutokubali
paa – enda juu
baa – janga
bahasa – sio ghali
bahasha – karatasi ya kutia barua
Mifano ya vitate
Mifano ya vitate
1. sisi – nafsi ya kwanza wingi
zizi – makao ya ng’ombe
2. pofu – asiyoona
povu – vipotopoto vya hewa
3. zabuni – uza kwa kushindania bei
sabuni – mchanganyiko wa kufulia na kuoge
4. sabiki – kuwa mbele, tangulia
shabiki – mtu apendaye jambo au kitu sana
5. lila – wema
lira – aina ya pesa
6. jibu – jawabu. Neno la kuitikia au kujibia
jipu – uvimbe mkubwa wenye usaha
7. acha – tengana na mtu, hali au kitu
asa – kanya, shauri
8. shati – vazi
sharti – lazima
9. mjuzi – mwenye ujuzi
mjusi – ugonjwa wa kutoka damu puani;
10. manda – kitu kinachoweza kushikika
mada – kiini cha jambo fulani
11. ndugu – Watoto wa ukoo mmoja
dungu – sehemu anayokaa rubani
12. taga – toa yai katika kiloaka
tagaa – tawi
13. nyati – aina ya mnyama wa porini
nyeti – enye ugumu
14. machi – mwezi wa tatu wa mwaka
mechi – mashindano ya mchezo.
15. sahibu – rafiki
shaibu – mzee mwanamume
16. tosa – tia kitu katika kitu kiowevu.
toza – kiko, chombo cha kuvutia tumbako
17. machozi – Matone yatokayo machoni
majonzi – hali ya kutokuwa na furaha.
18. bunge – Baraza la taifa la kutungia sheria
buge – Mtu aliyekatika kidole
19. ngeli – mpangilio wa makundi ya nomino
geli – mchezo wa watoto wa kurusha vijiti
20. shairi – mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum
shahiri – Waziwazi
shayiri – Aina ya nafaka