Methali |
---|
Maamkizi |
Heshima na adabu |
Vitate |
Semi na nahau |
Tashbihi |
Istiara |
Shada/takriri |
Tanakali |
Ushairi |
Vitendawili |
Tashbihi jozi |
Maswali kadirifu |
Tashbihi / Vifananisho
- Tashbihi ni fani inayotumika kulinganishia sifa za kitu kimoja na kingine.
- Tashbihi inapotumika, kiunganishi kama/mithili ya/ja hutumika.
- Usemi fananisho kwa matumizi ya 'kama'.
Mifano ya tashbihi.
1. Mchafu kama fuko.
Fuko (a-wa): mnyama kama panya mwenye macho madogo madogo, na huishi shimoni.
2. Safi kama mfua uji.
3. Mvumilivu kama mtumwa.
4. Mlafi kama fisi.
5. Mnafiki kama panya, nduma kuwili.
6. Mwaminifu kama njiwa.
7. Huzuni kama mfiwa.
8. Wasiwasi kama kuku mgeni, mwasi.
9. Kwenda pole kama kobe, konokono.
10. Mfupi kama mbilikimo.
11. Mrefu kama unju.
12. Mwenye bidii kama mchwa, nyuki.
13. Mwenye uzembe kama kupe, chaza, kozi.
14. Mwenye nguvu kama tembo/ndovu, kifaru.
15. Mjinga kama samaki.
16. Mjanja kama sungura, Abunuasi.
17. Mkali kama simbabuka.
18. Mwoga kama kunguru.
19. Mwenye maneno mengi kama chiriku.
20. Mnyamavu kama kaburi/mava.
21. Wazi kama mchana.
22. Tulia kama maji mtungini.
23. Furahi kama mama aliyepata mtoto salama salimini; tasa aliyepata mtoto; kibogoyo aliyeota jino; kipofu aliyetanabahi kuona.
24. Hasira kama za mkizi.
25. Bahati kama mtende; mwana aliyezaliwa Ijumaa.
26. -ngi kama njugu, mchanga ufuoni mwa bahari, siafu.
27. Adimika kama wali wa daku; barafu ya kukaanga; kaburi la baniani; kivuli cha nzi; maziwa ya kuku.
Adimika (kt): Kupatikana kwa uchache au kwa nadra.
28. Nata kama gundi (As sticky as glue).
29. Nukia kama ruhani.
30. Nuka kama kidonda, beberu, mzoga.
31. Tamu kama halua.
32. Tamu kama asali.
33. Chungu kama shubiri, subiri.
34. Weusi kama wa mpingo, kizimwili.
35. Weupe wa theluji – sio wa mtu.
36. -zito kama nanga.
Nanga (i-zi): kitu kizito, jiwe au chuma ambacho hufungwa kwenye kamba na kutoswa majini ili izuiwe chombo kisichukuliwe na maji.
37. -epesi kama unyoya.
38. Kubwa kama uwanja wa ahera, bahari.
39. -pole kama kondoo.
40. Majuto kama ya firauni.
Firauni (a-wa): Jina la cheo cha wafalme wa zamani, pia farao.
41. Kuiga kama kasuku.
42. Maringo kama tausi.
43. Tumainia kama tai.
44. Angua kicheko kama radi, jitu, fisi.
45. Baridi kama barafu.
46. Kigeugeu kama kinyonga/lumbwi.
47. Wivu kama joka la mdimu.
48. Fuatana kama kumbikumbi.
49. Sauti nzuri kama kinanda, ndege, malaika.
50. Mrembo kama malaika.
51. Kupenda kama moyo wa mtu.
52. Kutunza kama jicho la mtu.
53. Msahaulifu kama nyati.
54. Kuzurura kama mbwakoko.
55. Kutapatapa kama samaki atolewapo majini.
56. - pofu kama jongoo.
57. Tumbo kubwa kama kiriba.
Kiriba (ki-vi): a) Tumbo kubwa isio wa kawaida. b) Mfuko uliotengenezwa kwa ngozi ya mnyama, na hutumika kubebea maji au vitu vingine uowevu.
58. Paa kama moshi.
59. Imara kama chuma cha pua.
60. Maneno mengi kama chiriku.
61. Msiri kama kaburi.