Sehemu ya ufahamu hukusudiwa kumwezesha mwanafunzi ayataje yafuatayo:
• Uwezo wa kusoma ufahamu husika
• Uwezo wa kuelewa maudhui ya ufahamu
• Uwezo wa kutaja maana na matumizi ya maneno mbalimbali katika kifungu. (ufahamu)
• Uwezo wa kutaja funzo au ujumbe wa ufahamu.
Ni jambo wazi kuwa wanafunzi wengi hawafanyi vizuri sana katika kuyajibu maswali ya ufahamu.
Tatizo hili hutokana na ukosefu wa makini wakati wa kusoma ufahamu na hata wakati wa kuyajibu maswali yenyewe.
Je, wewe kama mtahiniwa unastahili kufanya yapi ili ufue dafu katika sehemu hii?
1. Soma kifungu cha ufahamu mara ya kwanza. Kusoma huku kutakuwezesha kuelewa kiasi maudhui kwenye kifungu.
2. Yasome maswali yaliyoulizwa.
3. Soma kifungu tena na kwa makini zaidi.
4. Rudia kusoma maswali.
5. Lisome kila swali kwa makini.
6. Tafuta jawabu la swali hilo katika ufahamu. Ni vizuri kuweka alama (katika (ufahamu) sehemu ambayo umepata jawabu la swali.
7. Hata baada ya kupata jawabu, “rudi” tena kwenye ufahamu ili kuhakikisha jawabu uliloteua ndilo sahihi zaidi.
8. Upatapo swali linalohitaji maana ya neno au sentensi katika ufahamu, unatakiwa usome neno hilo au sentensi hiyo ukizingatia jinsi ambavyo imetumika . Ukifanya hili kwa makini bila shaka utapata jawabu mwafaka au sahihi.
Kumbuka: Si lazima uwe ushaliona neno husika hapo awali ili uweze kuyaelewa maana yake. La hasha! Ukisoma ufahamu na hasa aya na sentensi ambapo neno husika limetumika, bila shaka utaelewa maana yake.
9. Mara kwa mara, kunayo maswali yanayohitaji kuelewa ujumbe wa ufahamu wote kwa jumla ili kuyajibu. Sharti basi uusome ufahamu na kuuelewa ujumbe unaoashiriwa.
10. Unapoulizwa kuteua kichwa mwafaka zaidi kwa ufahamu, sharti uweze kugundua ni ujumbe upi uliopewa umuhimu zaidi katika ufahamu. Iwapo utausoma ufahamu na maswali yake kwa makini huna sababu ya kufeli maswali ya sehemu hii.
Kifungu cha Kwanza
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali yanayofuatia.
“Hamjambo enyi nyote mliofika katika hafla hii? Mimi ni mheshimiwa Mambo. Ndimi mbunge wa eneo la Kamili. Nimefika hapa kutokana na mwaliko wa mbunge mwenzangu wa eneo hili la Tushauriane. “Lengo letu la kufika hapa ni kuchanga pesa za kugharimia mradi wa ujenzi wa madarasaya watoto wetu. Kama mjuavyo, serikali imeanzisha curriculum ya shule za msingi yasiyo ya malipo. Hatua hiyo imechangia watoto wengi wasajiliwe katika shule. Kama wahenga walivyonena hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Baadhi ya watoto wetu wamejipata wakisomea chini ya miti.
Nasi hatutaki hali hii iendelee. Ndiposa leo tupo hapa kuchanga pesa. Ni wajibu wetu kusaidia ujenzi wa madarasa. Tusisubiri serikali itufanyie kila jambo. Halikadhalika, tukibebwa tusilevyelevye miguu. Tukishirikiana, bila shaka tutafua dafu. Tukumbuke kuwa umoja ni nguvu.” Alikonga roho kwa funda la maji kisha akaendelea. “Hatuna budi kuhakikisha kuwa watoto wetu wamepata elimu bora kwani elimu ni mwangaza. Ni mwangaza wa kumulika tunakoelekea. Tukiwapa watoto wetu elimu, siku za usoni watakuwa watu wa kutegemewa wala sio wa kutegemea. “Hata hivyo, elimu pekee haitoshi. Sharti tuwahimize wanetu wawe na heshima na nidhamu. Nidhamu ikikosa kwa watoto wetu, elimu yao itakuwa bure bilashi. “Nasi wavyele sharti tuwe vielelezo kwa watoto wetu. Tuzingatie mienendo na matendo mema. Tuelewe kuwa mwana hutazama kisogo cha nina.
Sijui ni kwa nini wahenga hawakusema kisogo cha baba”, umma uliangua kicheko. “Nanyi watoto kamwe msijigeuze kuwa punda ambaye fadhila zake ni mashuzi. Sharti mwonyeshe shukrani kwa wema mnaotendewa. Shukrani zenu mtazionyesha kwa bidii curriculumni, nidhamu ya kiwango cha juu na uajibikaji. Kamwe msiingilie anasa. Anasa ni pingu. Epukeni anasa na muipe elimu yenu kipaumbele. Kumbukeni mwangata mbili moja humponyoka. Elimu ikiwaponyoka, mtajiuma vidole mnamo siku za usoni. “Vilevile, ni vizuri nyinyi vijana mjue kuwa, mnatembea katika njia iliyo katikati ya bahari na moto. Upande mmoja upo moto wa ukimwi, upande ule mwingine ipo bahari ya dawa za kulevya. Sharti mtembee kwa uangalifu pasi kwenda kombo la sivyo … “Kama nilivyokuwa nimenena hapo awali, lengo kuu la kukutana hapa ni kuchanga pesa. Nitupapo macho pale maegeshoni, siyaoni magari mengi.
Hata hivyo, hilo halinivunji moyo. Ninaelewa kuwa, kutoa ni moyo usambe ni utajiri. “Sasa ni wakati wa kuchanga pesa. Kila mja alete alicho nacho; kiwe kidogo au kikubwa. Tukumbuke kuwa haba na haba hujaza kibaba na tembe kwa tembe huwa mkate. “Karibuni katika mchango, asanteni”
Maelezo ya msamiati
konga roho – meza maji kidogo kupunguza kiu
1. Maelezo ya kifungu hiki ni; a) hadithi b) riwaya c) hotuba d) ripoti
2. Mnenaji alikuwa mbunge wa eneo la a) Tushauriane b) Kamili c) shule d) hatujaelezwa
3. Ni maelezo yapi sahihi zaidi kulingana na kifungu?
4. Tukibebwa tusilevyelevye miguu ina maana
5 . Mnenaji aliwatahadharisha wazazi dhidi ya:
6. Mnenaji anaonekana:
7. Ni sahihi kusema:
8. Mnenaji anawashauri watoto wawashukuru wazazi wao kwa:
9. Kulingana na kifungu hiki ni zipi hatari kuu zinazowakabili vijana?
10. Ni maelezo yapi sahihi zaidi?