Kifungu cha 4

Kifungu cha nne: Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yatakayofuatia

Nilikuwa nimefika katikati ya gongo la msitu ule. Kwa zaidi ya saa nne, nilikuwa nikihangaika huku nimekanyaga chechele. Mavazi yangu yalikuwa yamerarukararuka kutokana na miba. Magotini na hata viganjani nilikuwa na majeraha kwa kuanguka maweni! Tayari nilikuwa nimepoteza pochi yangu. Sauti nayo ilikuwa imepotea kutokana na kulia na kupiga kamsa. Nilikuwa nikimlilia ndugu yangu mlungizi.

Safari yetu ya kuelekea kwa nyanya ilitumbukia nyongo tulipoamua kuifuata njia ya mkato. Njia ya msituni. Haraka yetu ikatuingiza matatizoni; kumbe haraka haraka haina baraka! Ghafla, nilisikia mluzi wa ajabu. Kufumba na kufumbua, nilimwona nyoka mkubwa ajabu mbele yangu. Moyo wangu ulinipapa kama kwamba ulitaka kufunguliwa utoroke. Macho yakanitoka pima kama ya panya aliyenaswa mtegoni. Nilijaribu kupiga kamsa lakini nikashindwa.

Nikawa kama mtu aliyeng’olewa ulimi. Nilipigwa na butwaa zaidi nyoka yule alipoanza kunizungumzia. Lo! Yapi haya? Tangu lini nyoka akaongea? Nilibaki pale kama mtu aliyepandwa. Miguu yangu nikaihisi ikiwa mizito kuliko nanga. Nyoka yule alitoa sauti ya ajabu na baada ya muda wa bana banua, vijoka vingi ajabu vikafika. Bila kukawia, vilinirukia na kuanza kuyatafuna mavazi yangu. Ole wangu! Punde, koti lile la kuazima likawa halipo tena. Hata viatu vyangu vilitokomea kwa kasi vinywani mwa vijoka vile.

Nilizidiwa na kuanguka chini pu! La kuanguka halikunipa nafuu. Vijoka vile vilianza kuzitafuna nywele, kope na nyusi kichwani mwangu. Dakika chache baadaye kichwa changu kilimeremeta kama kioo juani. Kisha vijoka vile vilikipaka mate nao mwasho ukawa haumithiliki. Mateso hayo yalipoisha vijoka vile viliniondokea na kutokomea.

Sijui nilikopata nguvu kiasi. Niliinuka na kuuponda wa fisi ili kujisalimisha. Lahaula! Lakwata! Kumbe joka lile lilikuwa na uwezo wa kupaa angani. Lilipaa na kunigonga kichwani kwa kishindo. Ghafla vijoka vile vikatokea tena. Kila kijoka kilitumbukiza kila kidole changu kinywani. Vidole vyote vya miguuni na mikononi. Nilijaribu kupiga kamsa lakini vijoka viwili ambavyo vilisalia bila kidole kinywani viliziba kinywa changu kwa mikia yao. Vijoka vingine viwili zaidi viliziba pua yangu. Sasa kila kijoka kilikuwa na wajibu wa kunitesa. Mkubwa wao naye alionekana kuridhika na kazi yao. Nusura nizimie kutokana na ukosefu wa hewa. Nilijikaza na kwa nguvu za ajabu nikavitingiza vijoka vile na kuvirusha mbali. Nilitimua mbio kama duma. Lo! Niligonga kiambaza kwa kishindo na kuanguka sakafuni. Nilianza kupiga unyende. Kote kulikuwa giza totoro.

  •  Miguu yangu nikaihisi ikiwa mizito kuliko nanga ina maana:
  1.  Mhusika alikuwa mgonjwa miguu.      
  2.   Mhusika alishtuka kiasi cha kutoweza kutoroka.
  3.  Mhusika alishtuka kiasi cha kutoweza kusimama.  
  4.   Mhusika alikuwa mzembe.
  •  Kulingana na kifungu, mhusika alijaribu kutoroka mara ngapi?
  1. Moja.    
  2.  Mbili.      
  3.  Tatu.          
  4.   Nne.
  • Kwa jumla nyoka wote walikuwa wangapi?  
  1.  Kumi na wanne.    
  2.  Kumi na mmoja.      
  3.  Ishirini na wawili.    
  4.  Ishirini na watano.
  • Ni maelezo yapi sahihi kulingana na kifungu?
  1. Mhusika alijeruhiwa kipajini na nyoka.  
  2. Mama yake mhusika alikuwa msituni.    
  3. Mhusika alipigana na nyoka kitandani. 
  4. Mama yake mhusika alikuwa ameshika taa.

10. Kichwa kinachofaa zaidi kwa taarifa hii ni:  

  1. Jinamizi.      

  2.  Safari ya kutisha.  
  3.    
      Nyoka wa ajabu.      

  4.    Kupotea njia.

Nilimwona mama akiwa na kandili mkononi. Aliniinua na kuanza kunipatia huduma ya kwanza. Kipaji changu kilikuwa kikivuja damu kwa wingi. Mto na mablanketi vilikuwa sakafuni. Mtu angedhani palikuwa na vita kitandani.

Maelezo ya msamiati

  • mluzi – sauti nyembamba ya pumzi inayotoka baina ya midomo miwili iliyobanwa na kuacha nafasi ndogo; sauti itolewayo na nyoka
  • kiambaza – ukuta

 

  •  Kwa nini mwandishi alikuwa akihangaika mle msituni?

a. Alikuwa amepotea njia.   b. Alikuwa na njaa.   c. Alikuwa ameshambuliwa. d. Alikuwa na wasiwasi.

  •  Mwandishi alikusudia kwenda wapi?

a. Msituni. b. Kwa bibiye. c. Kwa nduguye. d. Hatujaelezwa.

  •  Mluzi aliousikia ulikuwa wa nani?

a. Nduguye.    b. Vijoka.          c. Nyoka.          d. Mwindaji.

 

  •  Lipi lililokuwa la ajabu zaidi kuhusiana na nyoka yule?
  1.  Aliweza kuongea kama binadamu          
  2.  Alikuwa mkubwa ajabu.
  3. Alikuwa na vijoka vingi.                
  4.  Alikuwa na mbio sana.

 

  •  Kulingana na kifungu, yaelekea mwandishi baadaye angelazimika afidie nini?
  1. Viatu.    
  2.  Bombo.      
  3.   Koti.        
  4.   Pochi.